FIFA yaipiga marufuku Sierra Leone kushiriki michuano ya kimataifa kwa madai kuwa Serikali inaingilia Shirika hilo

FIFA yaipiga marufuku Sierra Leone kushiriki michuano ya kimataifa kwa madai kuwa Serikali inaingilia Shirika hilo

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Shirikisho la kimataifa la mpira wa miguu, FIFA limetangaza marufuku kwa Sierra Leone kushiriki mashindano ya soka ya kimataifa kutokana na madai ya uingiliaji wa serikali ya taifa hilo katika masuala ya michezo.

Uamuzi huo umekuja baada ya FIFA hivi karibuni kumtumia barua waziri wa michezo wa Sierra Leone kumueleza wasiwasi wake juu ya kufutwa kazi kwa rais wa Shirikisho la Soka la Sierra Leone (SLFA) Isha Johanes pamoja na katibu mkuu wake Christopher Kamara.

FIFA imesema marufuku hiyo itaondolewa pale SLFA na uongozi wake unaotambulika watakapoihakikishia kwamba inadhibiti shughuli za shirikisho hilo la soka na sio serikali ya Sierra Leone.

Marufuku hiyo inaamnisha Sierra Leone imepoteza haki zote za uanachama, na klabu zake za kitaifa haziwezi tena kushiriki katika mashindano ya kimataifa.
 
Ukichunguza Sana utakuta adhabu zote za fifa zinaelekezwa Africa tu sijui kwa nini sijawahi kusikia nchi za ulaya zimefanyiwa hivi' rejea world cup ni Africa tu zlitumika zile machine zao 📺
 
Ukichunguza Sana utakuta adhabu zote za fifa zinaelekezwa Africa tu sijui kwa nini sijawahi kusikia nchi za ulaya zimefanyiwa hivi' rejea world cup ni Africa tu zlitumika zile machine zao [emoji342]
Sasa serikali kuingilia masuala ya soka na Fifa kuingilia kati na kutoa adhabu ama wajirekebishe wewe unasema ni kuonea waafrika kwahyo unataka mashirikisho ya soka afrika yaongozwe na serikali zao?
 
Sasa serikali kuingilia masuala ya soka na Fifa kuingilia kati na kutoa adhabu ama wajirekebishe wewe unasema ni kuonea waafrika kwahyo unataka mashirikisho ya soka afrika yaongozwe na serikali zao?
Chama cha soka Africa caf kilitoa maamuzi gani Labda tuanzie hapo
 
Back
Top Bottom