beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Shirikisho la kimataifa la mpira wa miguu, FIFA limetangaza marufuku kwa Sierra Leone kushiriki mashindano ya soka ya kimataifa kutokana na madai ya uingiliaji wa serikali ya taifa hilo katika masuala ya michezo.
Uamuzi huo umekuja baada ya FIFA hivi karibuni kumtumia barua waziri wa michezo wa Sierra Leone kumueleza wasiwasi wake juu ya kufutwa kazi kwa rais wa Shirikisho la Soka la Sierra Leone (SLFA) Isha Johanes pamoja na katibu mkuu wake Christopher Kamara.
FIFA imesema marufuku hiyo itaondolewa pale SLFA na uongozi wake unaotambulika watakapoihakikishia kwamba inadhibiti shughuli za shirikisho hilo la soka na sio serikali ya Sierra Leone.
Marufuku hiyo inaamnisha Sierra Leone imepoteza haki zote za uanachama, na klabu zake za kitaifa haziwezi tena kushiriki katika mashindano ya kimataifa.