Vawulence
JF-Expert Member
- Jan 4, 2009
- 1,930
- 2,118
Rais wa Shirikisho la Kimatiafa la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), Gianni Infantino ameipongeza timu ya Simba kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa 2020/2021.
Katika barua yake kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia, Rais Infantino alisema kuwa ubingwa ni matokeo ya juhudi na kutekeleza majukumu kwa kila mmoja ndani ya klabu hiyo.
"Naomba uwasilishe pongezi zangu kwa kila mtu aliyehusika katika mafanikio ya Simba SC, na kuwatia moyo waendelee kufanya kazi kwa moyo wa ushirikiano, ari na ushupavu" alisema Rais Infantino katika barua yake.
Pia alimshukuru Rais Karia wa (TFF) kwa kuchangia maendeleo na ustawi wa Mpira wa Miguu katika ukanda huu na Duniani kwa ujumla.
IMEANDIKWA NA DAUDI ELIBAHATI