FIFA yajadili uwezekano wa kubadilisha muda wa kufanyika kwa kombe la dunia

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Shirikisho la soka duniani FIFA, linaongoza kikao kwa njia ya mtandao, kujadili uwezekano wa kipindi cha kufanyika kwa kombe la dunia, kubadilishwa kutoka baada miaka minne hadi miwili.

Wakuu wa soka kutoka nchi 211 wanashiriki katika mkutano huo, utakaangozwa na rais wa FIFA Gianni Infatino.

Infatinno, akizungumza mwezi Novemba jijini Cairo, alipohudhuria mkutano mkuu wa Shirikisho la soka barani Afrika alisema wanaopinga mpango huo, wanaogopa mabadiliko katika mchezo huo.

Tayari CAF imesema inaunga mkono mabadiliko hayo, lakini mashirikisho ya soka barani Ulaya na Kusini mwa America, yanapinga kwa kile ambacho wakuu wa soka katika mashirikisho hayo wanaona, mpango huo utarudisha nyuma maendeleo ya soka na kuathiri mashindano mbalimbaki katika bara hilo.

RFI Swahili
 
Shirikisho la soka duniani FIFA, linaongoza kikao kwa njia ya mtandao, kujadili uwezekano wa kipindi cha kufanyika kwa kombe la dunia, kubadilishwa kutoka baada miaka minne hadi miwili.
Hiyo kitu ni ngumu na vilabu vingi ulaya vimepinga
 
Wataharibu ladha ya mashindano, siku hizi wanatengeneza mambo mengi yasiyo na maana, wanataka kuufanya mpira wa miguu uwe kama playstation.

Juzi tu wameongeza timu zinazoshiriki, leo wanataka kupunguza muda, mwishowe kombe la dunia litakuwa kama ligi ya dunia, lichezwe kila msimu.
 
Wallace Karia anasemaje kuhusu hili suala ?
 
FIFA ndio wanaharibu mchezo wa soka, kwanza huko nyuma walianza kwa kuleta sheria nyingi za kipuuzi eti kulinda mastaa na matokeo yake mchezo wa mpira ukawa na firimbi nyingi pamoja na kadi kibao tofauti na zamani.

Kumekuwa na matukio ya wachezaji kukosa mechi kwa kile kinachoitwa kulimbikiza kadi za njano wakati inajulikana wazi kwamba mchezo wa soka sio sawa na mchezo wa tennis.

Sasa leo wamezuka tena na hili la kombe la dunia eti lichezwe kila baada ya miaka miwili..!! Sasa hao wachezaji wamekuwa ni robot au wanadamu.

Nini faida ya haya mashindano kufanyika kila baada ya miaka miwili badala ya minne kama ilivyo sasa. Hawaoni kwamba haya mashindano yatakosa hata maana na ile ladha inayoambatana nayo yanapofanyika kila baada ya miaka minne.

Ni vema FIFA wafahamu kwamba, kuchamba kwingi ni kushika mavi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…