FIFA yakataa ombi la Iran la kucheza mechi za Kombe la Dunia nje ya Marekani

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
FIFA imeripotiwa kukataa pendekezo la Iran la kuhamisha mechi zake za Kombe la Dunia 2026 kutoka Marekani hadi Mexico.

​
Ombi hilo limekuja baada ya Maofisa wa Iran kuibua wasiwasi wa kiusalama na kueleza upendeleo wa kuepuka kucheza kwenye ardhi ya Marekani huku kukiwa na mvutano wa kisiasa wa kijiografia.

Licha ya kutokuwa na uhakika juu ya ushiriki, Iran hatimaye ilithibitisha kwamba bado ina nia ya kushiriki katika Mashindano hayo.

Soma zaidi: Iran yataka kucheza mechi za Kombe la Dunia nje ya Marekani

​
Kwa mujibu wa habari, FIFA haina mpango wa kubadilisha Viwanja vilivyopangwa vya Los Angeles na Seattle. Maofisa wanaamini kuwa hatua kama hiyo haitawezekana kwa kuwa tiketi tayari zimeuzwa na kubadilisha maeneo kutaleta matatizo ya kiufundi kwa timu nyingine kwenye kundi.

Iran italazimika kucheza mechi zake huko Merekani kama ilivyopangwa hapo awali.

====

FIFA has reportedly rejected Iran’s proposal to move its World Cup 2026 matches from the United States to Mexico. The request came after Iranian officials raised security concerns and expressed a preference to avoid playing on American soil amid ongoing geopolitical tensions.

Despite earlier uncertainty about participation, Iran ultimately confirmed that it still intends to take part in the tournament.

According to reports, FIFA has no plans to change the scheduled venues in Los Angeles and Seattle. Officials believe such a move would be impractical since tickets have already been sold and altering the locations would create logistical complications for other teams in the group.

As a result, Iran will likely have to play its matches in the United States as originally planned.
 
hiyo inaitwa ni kusuka au kunyoa.. kuwa na mkono wa birika au wakutoa.. kujenga taifa au kubomoa.. kugawanya kujumlisha kuzidisha au kutoa ,chagua moja!
 
Iran waende CAS rais wa sasa wa Fifa ni kibaraka wa Trump
 
Hao FIFA ni wapumbafu. Hivi waliona ni sahihi kuiweka Iran na Marekani kundi moja? Au kuna kitu walikipanga tangu zamani kwa timu ya Iran? Wanataka wawafanye nini hao wachezaji na mashabiki kutoka Iran?
 
hiyo inaitwa ni kusuka au kunyoa.. kuwa na mkono wa birika au wakutoa.. kujenga taifa au kubomoa.. kugawanya kujumlisha kuzidisha au kutoa ,chagua moja!
Uwe na mkono wa Sweta au ukatwe suna 🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…