Ila FIFA kwahiyo migogoro ya kisiasa ndio unahalisha ubaguzi wa kimechezo kama huu tena toka miaka 1980...
======
Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) limepiga marufuku waamuzi wa kimataifa kutoka nchini England, Anthony Taylor na Michael Oliver, kuchezesha mchezo wowote unaoihusu timu ya taifa ya Argentina katika michuano ya Kombe la Dunia inayooendelea.
Hatua hiyo ya FIFA inakuja kufuatia muendelezo wa misingi ya kisiasa na kidiplomasia inayohusisha mgogoro wa kihistoria wa Visiwa vya Falkland (Falkland Islands) kati ya Uingereza na Argentina, uliosababisha vita kubwa mwaka 1982.
Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na gazeti la The Independent, FIFA imesisitiza msimamo wake wa kutofungamana na upande wowote katika masuala ya kijiografia na kisiasa (geopolitical neutrality).