Magoli ya kiungo mshambuliaji Abdelhamid Sabiri anayeichezea Sampdoria ya Italia na Zakaria Aboukhlal wa Toulouse ya Italia yameipa ushindi #Morocco na kuweka matumaini ya kufuzu Hatua ya Mtoano kutoka katika Kundi F.
Morocco ambayo ni timu ya pili ya Afrika kupata ushindi katika michuano hiyo baada ya #Senegal, imefikisha pointi 4 katika mechi mbili ikisaliwa na mchezo mmoja dhidi ya Canada.