SoC04 Fikra bunifu kuboresha Sekta ya Afya kwa miaka 5 hadi 25 ijayo

SoC04 Fikra bunifu kuboresha Sekta ya Afya kwa miaka 5 hadi 25 ijayo

Tanzania Tuitakayo competition threads

Ahuche

New Member
Joined
May 21, 2024
Posts
2
Reaction score
0
Zifuatazo ni changamoto kuu zinazopaswa kushughulikiwa ndani ya kipindi Cha miaka 5-25:
1. Upungufu wa watumishi wa Afya
Changamoto:

Tanzania inakabiliwa na upungufu mkubwa wa madaktari,wauuguzi,na wataalamu wa Afya kutokana na idadi kubwa ya wagonjwa na idadi ndogo ya wahudumu

Mikakati ya kutatua:
. Kupanua program za mafunzo ya Afya:
kuongeza idadi ya vyuo vya tiba na programu za mafunzo Kwa wataalamu wa Afya.

. Kutoa motisha Kwa watumishi: kutoa motisha Kama vile mishahara Bora,mazingira mazuri ya kazi na fursa za mafunzo ya juu ili kuvutia na kuweka watumishi wa Afya.

. Kuwapatia mafunzo maalumu wafanyakazi wa ngazi za chini ili waweze kutekeleza baadhi ya majukumu ya kitaalamu.

. Kuongeza ufadhili na rasilimali:Serikali na wadau wa Afya wanapaswa kuongeza bajeti sekta ya Afya ili kuwezesha kuajiri watumishi wapya na kutoa mafunzo Kwa wataalamu wa Afya. Utafutaji wa fedha za ziada kutoka Kwa wahisani na mashirika ya kimataifa ili kusaidia programu za mafunzo na ajira Kwa watumishi wa Afya

2. Miundombinu duni ya Afya

Changamoto:
. Ukosefu wa vifaa vya kisasa,majengo yasiyotosheleza na mazingira duni ya kazi katika vituo vingi vya Afya nchini

Mikakati ya kutatua:
. Kujenga na kukarabati vituo vya Afya:kuwekeza katika ujenzi na ukarabati wa hospitali,vituo vya Afya na zahanati

. Kusambaza vifaa vya kisasa: kuweka vifaa vya kisasa na vya kutosha katika vituo vya Afya,ikiwa ni pamoja na mashine za uchunguzi,vitanda vya wagonjwa na vifaa vya upasuaji.

. Kushirikiana na sekta binafsi: kushirikiana na sekta binafsi ili kupata rasilimali na utaalamu wa kuboresha miundombinu ya Afya

3.Upatikanaji mdogo wa huduma za Afya vijijini

Changamoto:

Wananchi wengi wa vijijini wanapata huduma duni za Afya kutokana na umbali wa vituo vya Afya na uhaba wa watumishi na vifaa

Mikakati ya kutatua:
. Kliniki tembezi au jogefu:kuanzisha kliniki zinazotembea ili kufikisha huduma za Afya Kwa maeneo yasiyofikika kwa urahisi.

. Matumizi ya teknolojia ya mawasiliano(telemedicine):kutumia teknolojia ya telemedicine ili kuruhusu madaktari kutoa huduma na ushauri Kwa wagonjwa wa vijijini bila kuwapo kimwili au kuonana ana Kwa ana.

. Ujenzi wa vituo vya Afya vijijini: kujenga vituo vya Afya katika maeneo ya vijijini na kutoa motisha Kwa wahudumu wa Afya kufanya katika maeneo haya.

4. Magonjwa yasiyo ya kuambukiza

Changamoto:
. Ongezeko la magonjwa yasiyo ya kuambukiza Kama vile kisukari,shinikizo la damu ,saratani, magonjwa ya Figo na magonjwa ya moyo.

Mikakati ya kutatua:
. Elimu na uhamasishaji:kuendesha kampeni za kitaifa za kuelimisha wananchi kuhusu hatari na Kinga ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

. Upimaji na uchunguzi wa mapema:kuweka mipango ya Upimaji wa mapema na uchunguzi wa mara Kwa mara ili kugundua na kushughulikia magonjwa haya katika hatua za awali.
. Programu za lishe na mazoezi:kukuza proragamu za lishe bora na mazoezi ya mwili kama njia za kuzuia magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

5. Ukosefu wa bima ya Afya Kwa wote

Changamoto:
. Idadi kubwa ya wananchi hawana bima ya Afya hivyo wanashindwa kumudu gharama za matibabu.

Mikakati ya kutatua:
. Kuanzisha na kuimarisha mpango wa bima ya Afya Kwa wote ili kuhakikisha Kila mwananchi anapata huduma Bora za Afya bila kikwazo Cha kifedha.

. Mikopo na mifuko ya Afya ya jamii:kuanzisha mifuko ya Afya ya jamii na Mikopo nafuu ya bima ya Afya ili kuwezesha wananchi wengi zaidi kujumuishwa.

6.Upatikanaji wa dawa na vifaa tiba

Changamoto:
. upungufu wa dawa muhimu na vifaa tiba katika vituo vya Afya hali inayoathiri utoaji wa huduma Bora za Afya.

Mikakati ya kutatua:
. Mifumo Bora ya ugavi: kuweka Mifumo Bora ya ugavi wa dawa na vifaa tiba ili kuhakikisha upatikanaji wake Kwa wakati na Kwa gharama nafuu.

. Uzalishaji wa ndani: kujenga viwanda vya kuzalisha dawa na vifaa tiba ili kupunguza utegemezi wa bidhaa za nje na kupunguza gharama za uagizaji.

7. Changamoto za Afya ya akili

Changamoto:
. Huduma za afya ya akili Bado ni duni na hazipewi kipaumbele,huku idadi ya watu wanaosumbuliwa na matatizo ya akili ikiongezeka.

Mikakati ya kutatua:
. Elimu na uhamasishaji: Kuendesha kampeni za kitaifa za kuelimisha umma kuhusu Afya ya akili na kuondoa unyanyapaa uanaoambatana na magonjwa ya akili.

. Kuongeza rasilimali Kwa Afya ya akili:kuwekeza katika vituo vya Afya ya akili na kutoa mafunzo Kwa wataalamu wa Afya katika eneo hili.

. Huduma za ushauri Nasaha: Kuanzisha na kukuza huduma za ushauri Nasaha na tiba ya kisaikolojia katika vituo vya Afya na shule.

Kwa kushughulikia changamoto hizi kwa mbinu na mikakati iliyoainiahswa, Tanzania inaweza kuboresha sana sekta yake ya Afya na kufikia viwango vya kimataifa,hivyo kutoa huduma Bora za Afya Kwa wananchi wake wote.
 
Upvote 1
Ujenzi wa vituo vya Afya vijijini: kujenga vituo vya Afya katika maeneo ya vijijini na kutoa motisha Kwa wahudumu wa Afya kufanya katika maeneo haya.
Sawa sawa.


Idadi kubwa ya wananchi hawana bima ya Afya hivyo wanashindwa kumudu gharama za matibabu.
Hapa niko na swali: Je? Bima ya afya ni Bure?

Uzalishaji wa ndani: kujenga viwanda vya kuzalisha dawa na vifaa tiba ili kupunguza utegemezi wa bidhaa za nje na kupunguza gharama za uagizaji.
Nzuri, tujijengee uwezo wa kujitegemea kiafya na mambo yote tu.
 
Sawa sawa.



Hapa niko na swali: Je? Bima ya afya ni Bure?


Nzuri, tujijengee uwezo wa kujitegemea kiafya na mambo yote
Kuhusu bima ya Afya : nilizungumzia kuhusu mifuko wa kitaifa wa bima ya Afya ambao mwananchi atalazimika kuchangia kiasi kidogo Kwa kipindi Fulani na mfumo huo utakuwa na jukumu la kugharamia matibabu ya wananchi wote
 
Kuhusu bima ya Afya : nilizungumzia kuhusu mifuko wa kitaifa wa bima ya Afya ambao mwananchi atalazimika kuchangia kiasi kidogo Kwa kipindi Fulani na mfumo huo utakuwa na jukumu la kugharamia matibabu ya wananchi wote
Yas atachangia, hapo hiyo ni nzuri ili kuibakiza heshima ya huduma za afya na kujali afya.

Hili likienda na elimu ya afya bure inayopatikana kwa wote itapendeza sana. Bima nzuri ni kujikinga.
 
Back
Top Bottom