DENG XIAOPING
JF-Expert Member
- Mar 6, 2022
- 2,396
- 2,598
FIKRA
FIKRA CHANYA
- Ni wazo au ni mkusanyiko wa mawazo ndani ya ubongo wa mtu yaliyo na matokeo chanya. Fikra chanya huhusisha kufikiri kwa makini juu ya jambo fulani kwa kuzingatia njia na matokeo chanya juu ya jambo fulani mfano fikra chanya juu ya ujenzi wa miundombinu bora ya barabara ili kuepusha ajali za mara kwa mara.
FAIDA ZA FIKRA CHANYA [ VIJANA, WATU WAZIMA, VIONGOZI, JAMII ]
VIJANA
- Fikra chanya huchochea zaidi maendeleo miongoni mwa vijana endapo zikitiliwa zaidi mkazo na vijana.
- Fikra chanya husaidia kumwepusha kijana na tabia hatarishi kwa afya ya mwili wake mfano ulevi, matumizi ya madawa ya kulevya n.k
- Fikra chanya huweza kumsaidia zaidi kijana kutimiza ndoto na mipango mbalimbali yenye manufaa kwake aliyo panga.
WATU WAZIMA
- Fikra chanya miongoni mwa watu wazima huweza kuchangia kuwapo kwa jamii iliyo starabika kutokana na shauri zilizo jaa hekima na busara zinazo changizwa na fikra chanya ndani yao ambazo watu wazima watakuwa wanatoa kwa vijana na watoto kwenye jamii na hivyo kujenga jamii iliyo bora.
- Fikra chanya miongoni mwa watu wazima huchangia ujenzi wa familia zilizo bora kupitia malezi yaliyo bora yatakayo saidia kujenga kizazi kilicho bora.
- Fikra chanya pia husaidia kuwaepusha watu wazima na matukio yasiyo faa ndani ya jamii mfano ubakaji wa watoto kwa kuwa fikra chanya hupelekea heshima kujengeka Kati ya mtu na mtu.
VIONGOZI
- Fikra chanya miongoni mwa viongozi huchangia taasisi, kampuni, jamii, nchi n.k wanazo ongoza kupiga hatua kubwa za kimaendeleo kutokana na mawazo bora na mema viongozi watakayo kuwa Wanaya waza yatakayo pelekea utekelezwaji wake kuleta faida.
- Fikra chanya huchangia kuongezeka/kuwepo kwa uzalendo miongoni mwa viongozi juu ya nchi na rasilimali zake kwa kuwa wata kuwa wana iwazia nchi mema zaidi ya kimaendeleo.
- Fikra chanya huweza kuwa saidia viongozi kutatua matatizo mbalimbali yanazo zikabili sehemu wanazo ziongoza kama vile wilaya, mikoa, nchi, taasisi binafsi au za kiserikali mfano tatizo la kuyumba kiuchumi fikra chanya ndani ya kichwa cha kiongozi husaidia kujenga mbinu mbalimbali za namna ya kukabiliana na tatizo la namna hiyo na kuweza kulishinda.
JAMII/TAIFA
- Jamii iliyo nyuma kimaendeleo inahitaji watu waliobeba fikra chanya ndani ya vichwa vyao ili kuweza kuchochea mabadiliko na maendeleo ndani ya jamii kwa kuja na mbinu mpya ndani ya jamii za kukuza maendeleo ya jamii.
- Fikra chanya huweza kusaidia watu ndani ya jamii kujua umuhimu wa kulisaidia taifa katika maendeleo mfano ulipaji wa kodi kwa maendeleo ya taifa zima.
- Fikra chanya huchangia uwepo wa jamii iliyo starabika, yenye tabia zilizo njema, jamii yenye kujishughulisha na shughuli za kiuchumi zilizo halali zenye kukuza uchumi wa jamii na taifa hilo.
ATHARI ZA FIKRA HASI [ VIJANA, WATU WAZIMA, VIONGOZI, JAMII ]
VIJANA
- Vijana kwa kiasi kikubwa huathiriwa na yale mawazo mabaya yanayojenga fikra hasi vichwani mwao ambazo hupelekea wao kutenda yale yasiyo faa na kuwaingiza matatizoni mfano fikra hasi za kushiriki ngono zisizo salama katika umri mdogo jambo ambalo hupelekea mimba katika umri mdogo, pia wanaweza kupatwa na magonjwa hatarishi Kama UKIMWI.
- Fikra hasi huathiri na kudumaza utendaji wa kazi wa vijana waliowengi kwa kiwango kikubwa na hivyo kuleta matokeo hasi ya kazi zao.
- Fikra hasi huchangia kwa kiwango kikubwa kuzima ndoto na mipango ya vijana waliowengi yenye manufaa katika maisha yao.
WATU WAZIMA
- Fikra hasi hupelekea watu wazima kufanya mambo yasiyo faa kulingana na umri wao na hivyo heshima yao ndani ya jamii hupotea.
- Fikra hasi huweza kuchangia migogoro mbalimbali ya kifamilia ambayo huacha matokeo hasi yaliyo na madhara makubwa kama vifo, majeraha makubwa.mfano wivu ndani ya familia huchangia matatizo mengi makubwa.
- Fikra hasi huchangia umasikini mkubwa kwa watu ndani ya familia zao kwa kujihusisha na mambo yasiyo faa kama vile ulevi uliopindukia ambao huwa ni kikwazo kikubwa cha maendeleo katika familia nyingi.
VIONGOZI
- Fikra hasi kwa kiwango kikubwa huchangia uongozi mbovu kwa viongozi katika maeneo wanayo ongoza mfano nchi,kampuni,taasisi n.k
- Fikra hasi kwa kiongozi huweza kudumaza maendeleo ya taasisi, jamii anayo ongoza.
- Fikra hasi huweza kuathiri uwezo wa kifikra wa kiongozi na hivyo kushindwa kubuni njia mbadala na zilizo bora za kuweza kuwa ongoza na kuwa komboa watu anao waongoza kutoka katika dimbwi la umasikini.
JAMII/TAIFA
- Fikra hasi huweza kuchangia jamii au taifa kutokupiga hatua katika ngazi za uchumi, sayansi na maendeleo.
- Fikra hasi huchangia mmomonyoko mkubwa wa maadili katika jamii na taifa kiujumla.
- Fikra hasi ndani ya taifa au jamii huweza kusababisha utengano na ubaguzi miongoni mwa watu kwa misingi ya rangi, kabila, dini.
NJIA ZA KUJENGA NA KUKUZA FIKRA CHANYA [ NJIA ZA KUDHIBITI FIKRA HASI ]
- Usomaji wa vitabu na majarida mbalimbali ya kuelimisha huchangia kwa kiasi kikubwa mtu kuwa na fikra chanya zitakazo msaidia katika mambo mbalimbali.
- Mfumo wa elimu ulio bora hupelekea uzalishaji wa wasomi walio beba fikra chanya vichwani mwao, zitakazo saidia kupambana na matatizo yanayo sababisha jamii zao na taifa Katia kupata maendeleo yaliyo bora.
- Malezi yaliyo bora pia ni njia nzuri ya kujenga jamii iliyo beba fikra chanya zitakazo epusha jamii kutumbukia katika matendo mengi mabaya yaliyo na matokeo hasi mfano wizi, ubakaji.
- Marafiki walio wema na walio beba fikra chanya ni msaada tosha kwa vijana katika kupiga hatua za kimaendeleo, kutokana na aina ya ushauri bora mtakao kuwa mnapatiana baina yenu.
- Kujihusisha katika majukwaa na midahalo ya kuelimisha pia ni kichocheo kikubwa cha kujenga fikra chanya ndani ya mtu kutokana na maarifa mbalimbali mtu atakayo yapata katika midahalo hiyo.
- Matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii pia husaidia kukuza fikra chanya kwa watumiaji kwa kusoma na kujifunza mambo mbalimbali mitandaoni yaliyo ya kuelimisha husaidia mtumiaji kupata mawazo mapya kila mara yaliyo msaada kwake katika kukabiliana na changamoto mbalimbali mfano maarifa yapatikanayo kwenye mtandaoni wa kijamii wa JAMIIFORUMS.
- Kujiepusha na mambo mbalimbali yanayoweza kusababisha fikra hasi ndani yako zitakazo acha madhara makubwa mfano msongo wa mawazo madhara kama kujiua.
- Kujifunza kwa walio fanikiwa husaidia kukuza fikra chanya za mafanikio ndani ya mtu au watu.
- Asili ya neno fikra au fikira ni kutoka katika lugha ya kiarabu.
- Ni wazo au ujumbe uliojengeka katika ubongo wa mwanadamu ambao hupelekea utendaji wa Jambo fulani. Mfano fikra za ukombozi zilizo jengeka miongoni mwa Waafrika wakati wa kudai uhuru.

Upvote
5