Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 590
- 1,648
Fikra huru, kuwa na mawazo yako kuhusu mambo mbalimbali hasa kwenye mambo ya dini na siasa na sio kukubali tu kama vilivyowekwa, kuzoeleka au kufundishwa. Kuwa na fikra huru kumewaletea matatizo watu hawa kwasababu tu wamekuwa tofauti na vilivyokuwa na mizizi na kuzoeleka.
Baruch De Spinoza (1632 - 1677) ni mwanafilosofia wa kihayudi ambae mawazo yake yalikuwa tofauti na jamii yake. Japokuwa alisomeshwa katika misingi ya kiyahudi yenye kumuamini Mungu na kuamini katika kitabu kitakatifu cha bibilia, mawazo yake yalikuwa tofauti. Kadri alivyozidi kukua mawazo yake yalibadilika na kuwa tofauti kabisa na jamii yake japokuwa hakuwahi kusema wazi kwamba haamini kama kuna Mungu au anaunga mkono wayahudi wenzake bali yeye ni mtetezi imara wa Mungu. Baruch alisema japokuwa amesomeshwa katika misingi ya kiyahudi lakini mwishowe anawajibu wa kuheshimu mitazamo mengine
Kwenye kitabu chake cha The Ethics (1677) kilichoandikwa kwa kilatini alipinga moja kwa moja kanuni za wayahudi na dini kiujumla. Akisema mambo kama hakuna maisha baada ya kifo, mwanadamu sio kiumbe aliyechaguliwa na Mungu, Mungu haukumu wala hawapongezi watu wema na maisha baada ya kifo, Bibilia iliandikwa na watu wakawaida, Mungu sio fundi wala mjenzi wala mfalme au mwanamkakati wa kijeshi ambaye anawaita waumini kuchukua upanga mtakatifu na kwamba kila kitu katika kalenda ya kitamaduni ya kiliturujia ni ushirikina mtupu na upuuzi.
Kitabu chake hiki kilimfanya kuandikiwa barua ya kumpa laana kutokana na mawazo yake. Katika kumbadilisha mawazo yake Baruch alipewa ofa ya dola 500 kufundisha chuoni na aache msimamo wake wa kuongelea na kupingana na misingi ya kiyahudi lakini alikataa ofa hiyo. Kutokana na hayo Baruch alitengwa jamii yake sababu alioneka kama mtu mwenye laana. Sikuchache baada ya kutengwa kwake Baruch alikatwa na kisu shingoni katika jaribio la kumuua lililofanywa na waandamanaji waliokuwa wanachukia fikra zake. Baruch aliwahi kutoka eneo hilo hivyo kuwa na jeraha dogo amablo halikuwa na madhara makubwa sana, kutoka hapo akaanza kuamini kwamba kuna sehemu ambazo ni hatari kwa wanafilosofia kuishi na kuamua kuhama na kujitenga mbali na sehemu ya mizizi yake, ambako mpaka anafariki alikuwa ni mtu mpweke.
Vivyo hivyo kwa muandishi wa vitabu Salman Rushdie(1947) asiyefata misingi ya dini ya kiislam na asiyeamini kwenye uwepo wa Mungu, fikra zake zimefanya akafanyiwa jaribio baya kabisa la kumuua ambapo ni juzi tu hapa tarehe 12 August 2022 alichomwa kisu zaidi ya mara kumi. Japokuwa amekuwa akipokea vitisho mara kwa mara hili limekuwa jambo la kutisha kabisa kutokea kwenye maisha yake. Rushdie alizaliwa mjini Bombay (sasa Mumbai), India wiki nane kabla ya kukoma kwa utawala wa himaya ya waingereza. Rushdie amekulia kwenye familia ya dini ya kiislam ambayo hawakua wakifata misingi ya dini hiyo. Utoto wake alikua amezungukwa na marafiki wenye dini mbalimbali kama wahindu, waislamu, wasick na wakristo, haikuwa jambo kubwa kuchangamana na watu wa dini tofauti. Rushdie kama watoto wengine alikuwa kisomewa hadithi kabla ya kulala na baba yake. “The 1001 night” ndiyo kitabu baba yake alikuwa akimsomea, kitabu ambacho maudhui yake yalikuwa hayafai kuhadithiwa watoto lakini baba yake Rushdie alimuhadithia kwa namna ambayo ilifaa kwa Rushdie.
Usimuliaji huo ulikuwa wa aina yake kwa Rushdie ikawa chachu kwake kupenda kusoma vitabu na kutaka kuja kuwa mwandishi baadae. Ilikua akiulizwa unataka kuwa nani ukiwa mkubwa jibu lake lake lilikuwa moja tu, Mwandishi! Taratibu alianza kuandika vitabu japokuwa vilikuwa vidogo, na moja ya kitabu alichoandika akiwa mtoto ilikuwa ni “Over the Raibow”, kitabu ambacho aliandika baada ya kutoka kuangalia tamthilia ya “Wizard of Oz”. Hadithi ambayo ilikua inahusu kijana kama yeye kutoka jiji la Bombay aliekutana na viumbe wa maajabu.
Akiwa na umri wa miaka 12 wazazi wake waliona kumpa nafasi Rushdie kwenda kusoma Uingereza itakuwa ni jambo kubwa sana wanaloweza kumfanyia mtoto wao, maamuzi ya mwisho kama ataenda au hapana yalikuwa mikononi mwa Rushdie. Japokuwa Rushdie alikuwa amezoea mazingira ya Bombay na alikuwa na marafiki wengi alikubali kwenda Uingereza bila ya kusita sababu aliona nisehemu nzuri ya kukuwa kiuandishi, sehemu ambayo itamkaribisha kwa mikono miwili na kufanikiwa kirahisi. Jambo ambalo lilikuwa kinyume na alichotarajia, kwanza alifika majira ya baridi hilo likawa changamoto ukizingatia ametoka sehemu ya kitropiki lakini pia alikutana na ubaguzi mkubwa wa rangi kutoka kwa waingereza na kwa mara ya kwanza kujihisi kama “mtu wa nje”. Lakini pia haikuwa rahisi yeye kufanikiwa kama mwandishi baada ya kumaliza shule.
Rushdie alikuwa amefungamana na tamaduni mbili ambapo ilimuwia vigumu kuchora mstari kujua yeye ni nani na nini anatakiwa kuandika, hivyo kila alichokuwa akiandika kina makosa mengi na hakifai. Ilifika wakatati akaamua kurudi India kujitafuta ambapo alikaa miezi mitano na nusu na kurudi tena Uingereza. Safari ile ilikuwa ya kufungua macho sasa akajua nini anatakiwa kufanya, yeye ni nani na nini kinamhamasisha. Kufuatia ufunua huo akaandika kitabu kingine ambacho kilikuwa jaribio la mwisho, kama kisingefanikiwa basi angekata tamaa kuwa mwandishi. “Midnight’s Children” ndio kitabu ambacho kilimfungulia Rushdie milango ya mafanikio, akafanikiwa kuuza nakala zaidi ya milioni moja ulimwenguni na kitabu chake kikatafsiriwa kwenye lugha zaidi ya 50.
Mafaniko yakazidi kuongezeka Rushdie akaanza kuandika kitabu cha “Satanic Verses”, kitabu ambacho alitumia miaka mitano kukamilisha kukiandika, kipindi ambacho hakuna aliyeona dalili za kukuwa kwa misingi ya dini ya kiislam. Baada ya kukikamilisha kuandika kitabu chake, Rushdie aliwatumia baadhi ya marafiki zake nakala za kitabu chake watoe maoni yao. Wote waliosoma kitabu hicho walimtahadharisha Rushdai juu ya mzozo kitabu hicho kingeibua miaka ya mbeleni, inashangaza kuwa hata bwana Rushdie mwenye alifikiri hivi.
Rushdie alijua fika kitabu hiki hakitafurahiwa na watu wanaoamini katika dini na hata yeye mwenyewe hakufurahishwa kwa alichokiandika, kilichomfurahisha ni ujasiri wake wa kuweza kuandika kitabu hicho na ujasiri wa kwenda mbali zaidi kuliko vitabu alivyowahi kuandika kabla. Kati ya mambo yanayohusu kitabu chake ni pamoja na kushutumu unyanyasaji kwa wanawake na ukandamizaji wa kipimo cha wanawake kwenye uvumilivu na alitilia shaka kananu za imani ya kiislam.
Mwaka mmoja baada ya kuchapishwa kwa kitabu chake matatizo yakaanza, maandamo yalizuka kutoka nchi mbalimbali zenye asili ya kiaribu na ambapo kuna wafuasi wa dini ya kiisalmu wakidai kitabu cha Rushdie taswira mbaya isiyoendana na mtume anaewakilisha waislam. Mwaka mmoja baada ya kuchapishwa kitabu chake tarehe 14 February 1988 kiongozi wa dini ya kiislam kutoka Tehran Ayatollah Khomein alitoa amri ya dini na ahadi ya dola milioni tatu za kimarekani kwa wamumini wa dini ya Kiislamu ulimwenguni kote kumuua bwana Rushdie, yoyote aliyehusika kuchapisha kitabu hicho akijua maudhui yake na yoyote anaunga mkono maudhui hayo kwa kile alichodai maudhui ya kitabu cha Rushdie kinatoa shambumbulio la kukufuru kwenye uislam, mtume wao na Quran.
Hali ilikua mbaya zaidi ndani ya masaa ishirini na nne kutoka kuandikwa kwa amri hiyo, maandamano makali yalizuka sehem mbalimbali wakisema Rushdie ni lazima afe. Rushdie akenda mafichoni, ambapo alikuwa mafichoni kwa miaka kumi kwa msaada wa serikali ya Uingereza. Ndani ya miaka hii kumi Rushdie alikuwa akitumia jina bandia, aliepuka majaribio ya kutaka kumuua zaidi ya kumi tano na alihamishwa mahali pa kukaa mara 56. Hali ilikuwa mbaya kwani watu waliomsadia kuchapisha ama kuzindua kitabu chake walikuwa matatani pia. Baadhi ya watu waliouliwa kutokana hili ni Amnai wa Norway, Aziz Nasim na Hitosh Iragash ambaye alitafsiri kitabu cha Rushdie kwa lugha ya kijapani.
Japokuwa waliompiga Rushdie ni wengi wapo waliomuunga mkono ikiwemo mwandishi vitabu mashuhuri Stephen King kutoka Uiengereza ambaye aliwapa siku moja kampuni ya kuuza vitabu kurudisha vitabu vya “Sanitic Verses” la sivyo atasitisha uuzwaji wa vitabu vyake hapo, kampuni hiyo ilirudisha vitabu vya Rushdie siku iliyofuata. Rushdie aliendelea kupokea vitisho hata baada ya kiongozi aliyetoa amri ya kuuawa kwake kufariki, lakini pia kiongozi alifata baada ya Ayatolla aliendeleza amri ile ya kuuawa kwa Rushdie
Mwaka 1991 Rushdie alihamia New York, Marekani na mwaka 1992 alianzisha kampeni ya kutaka amri ya kuuliwa kwake iliyotolewa na kiongozi kutoka Irani ifutwe. Kampeni za kutafuta na kumuua Rushdie ziliendelea ambapo lilifanyika shambilio baya sana nchini Uturuki likiwa limemlenga Aziz Nesim ambaye alietafsiri kitabu cha Rushdie kwa kituruki, shambulio ambalo liliua watu 32. Shambulio hili ndio lilikuwa shambulio kubwa kufanywa kutokana na maudhui ya kitabu cha Rushdie ambae taratibu maisha yake yalianza kurejea kama zamani.
Mwaka 1998 serikali ya Iran na Uingereza ilifikia makubaliano ya kusitisha vitisho na amri ya kuuwa kwa Rushdie lakini waumini ya dini ya kiislam walisema kwao amri ya kuuliwa kwa Rushdie bado ipo palepale na ipo siku watatekeleza jambo hilo. Vyombo vya habari Iran wakaendelea kuongeza dau la kuuawa kwa Rushdie kutoka $500,000 2012 mpaka $600,000 2016 na waumini wa kiislam wakaongezea $3,000,000 kutoka katika kiasi alichoaidi Ayatollah alipotoa amri ya kuuliwa kwa Rushdie. Rushdie aliendelea na maisha yake ya kawaida New York hadi tarehe 12 August 2022 ambapo alishambuliwa na mwanaume mmoja jukwaani akiwa kwenye halfa aliyokuwa akitoa mafunzo kwa kuchomwa na kisu shingoni na tumboni kwa mara 15.
Hii ni mifano midogo sana ya gharama unayoweza kulipia kwa kuwa na mawazo tofauti na mifumo fulani au mawazo fulani ya watu yaliyokomaa na kukubalika kwa mda mrefu. Watu hawana budi kujifunza kukubaliana kutokukubaliana kwa amani, mtu akiwa na mawazo tofauti na wewe isiwe ishara ya wewe kumvamia na kusokomeza mawazo yako kwenye kichwa chake. Jenga hoja, angalia anasema nini uje na majibu mazito zaidi yanayothibitisha mawazo yako ni bora kulicho alichokisema. Kusakama mawazo ya mtu ni kosa lakini kushambulia mtu sababu amekupa changamato kwenye kitu unachoamini ni makosa zaidi, kutofautiana kwa mawazo kwa mawazo sio vita!