Natural justice
Member
- Aug 15, 2021
- 30
- 47
Ndg zangu watanzania, ninapenda kutoa maoni yangu kwa shirika la reli Tanzania na Zambia yaani Tanzania Zambia Railway( TAZARA).
Usafirishaji wa abiria umekuwa changamoto kubwa kutokana na ajali za mara kwa mara zinazozipata treni za mizigo na hivyo kupelekea treni za abiria kushindwa kufanya safari zake na kuleta usumbufu mkubwa kwa abiria hasa wa mbeya to dar, mbeya to morogoro au Moro to Dar.
Shirika hili halina mifumo ya kidigitali inayotuwezesha abiria kupata taarifa kama usafiri upo ama la so inabidi hadi ufike kwny vituo vyao na kama ndio ushapaki mabegi kwa ajili ya safari itabidi ulale kituo husika hadi treni itakapowasili muda usiojulikana.
Niliwahi kwenda moja ya ofisi zao kushauri mambo kadhaa wakabaki kunishangaa.
USHAURI
-TAZARA wawe na mifumo ya kijamii kutoa habari mf account Facebook, Twitter, no za Simu iwe rahisi kujua nini kinaendelea, mbona mabasi wameandika namb za simu kwny ticket?
-Mabango yao yamechakaa sana ktk station zao, waweke mapya ili yasomeke.
- Zile MBAO za matangazo wawe wanaandika taarifa na ziwe za kweli
-Muda! Muda! Muda! Ni muhimu wakazingatia muda, unaambiwa safari ni ijumaa usiku matokeo yake unasafiri jpili asubuhi, na hapo ushaaga nyumbani na tiketi unayo mkononi. Ni full kulala station.
-Wafanyakazi wawe na ukarimu kwa wateja aisee ni wakali kweli, unaweza uliza swali ukajibiwa kwa swali au mtu akauchuna
- Mkuu Kadogosa najua unahusika hapa miundombinu hasa mlimba hadi makambako ifanyiwe maboresho yamkini na kwingine pia watu wanaumia sana hasa wafanyabiashara wa bidhaa zinazoharibika, wanapata hasara.
Tanzania inajengwa na itajengwa na watanzania. Nipo tayari kusahihishwa kama nimekosea.