Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,478
- 3,659
Nimeona nianzishe uzi wenye mada za kufikirisha katika maandishi na kudadavua maana ya maandishi yenyewe. Kwa kuanza naanza na mada ya njaa.
Ni nadra kutokukubali kuwa kuna uhaba wa njaa ulimwenguni. Upembuzi anuai unaweza bainisha hili. Njaa ni hulka. Ni fursa ya mja kujiainisha kihisia mbele ya jamii kimahitaji. Njaa ya fikra na njaa ya mwili zote njaa. Fikra ni sehemu ya mwili usio na shibe. Kutokujua kuwa hujui unahitaji nini ni njaa. Fikra si tendo la hiari, ila unapotaka kuanza kuwaza kufikiri ni wazi kuwa wazo lililotunga kuwaza kufikiri linatokana na ombwe la sintofahamu katika mfumo wa ufahamu. Kuwaza ni suala mtambuka kama ilivyo kupambana na njaa. Tamaa ni upungufu wa shibe ya hisia. Tamaa si hulka bali ni matokeo ya hulka. Njaa inaonekana, inasikika, inahisiwa. Si sahihi kusema kuwa njaa si nzuri. Njaa ni heri. Njaa ni amani. Njaa ni silaha. Lakini pia njaa ni janga. Nini njaa yako?