Fikra tamanifu za makamanda

Fikra tamanifu za makamanda

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
94,296
Reaction score
122,540
Makamanda wamechanganyikiwa.

Hawajui kama wanaenda au wanakuja.

Sasa sikilizeni nyie makamanda [ingawa najua hamna uwezo mkubwa wa kufikiri kwa kutumia akili, lakini jitahidini kuelewa].

Ni hivi:

Rais Magufuli hatofikishwa huko kwenye mahakama ya kimataifa ya jinai.

Hatofikishwa kwa sababu hakuna sababu yoyote ile ya msingi, inayolazimu yeye kufikishwa huko na kushitakiwa.

Hizi kelele mnazopigishwa na huyo mgombea wenu wa 2025, Bob Amsterdam, ni fikra/ mawazo tamanifu tu.

Sina hakika kama mnalitambua hilo. Kwamba, hawezi kufikishwa huko.

Natambua ni kiasi gani fikra/ mawazo tamanifu [wishful thinking] yanavyoweza kumpa mtu faraja ya muda mfupi pindi apitiapo kipindi kigumu cha maumivu ya kihisia na kiakili.

Mawazo hayo tamanifu hutoa hifadhi ya faraja.

Na ndo maana mnapoona au mnaposikia sijui mwanaharakati gani wa Twitter amepeleka barua au sijui ushahidi huko kwenye hiyo mahakama ya kimataifa ya masuala ya jinai, mnafurahi, mnachekelea, bila hata kuangalia na kupima uhasilia na mwelekeo wa kile mnachokitaka, kutokea.

Mtu yeyote anaweza kutangaza kumshitaki yeyote yule au chochote kile, popote pale. Ukweli huo nadhani hamuuzingatii kwa uzito na u maanani unaostahili.

Licha ya kwamba Tanzania tuna matukio ya hapa na pale ya ukiukwaji wa haki za kibinadamu, bado hatujafikia viwango vya kushitakiwa rasmi kwenye hiyo mahakama.

Najua nyie makamanda huwa hampendi kuambiwa ukweli. Mnachokipenda ni maneno ya kufarijiana tu mpaka uchaguzi ujao.

Na uchaguzi ujao ukifika, haya ya 2020 mtakuwa mshayasahau kama ambavyo mmeyasahau yote ya 2015, 2010, 2005, 2000, na 1995.

Hivyo endeleeni kuota ndoto za mchana. Si Raisi Magufuli, Da Samia, Bw. Majaliwa, au Kamanda Sirro atayetiwa pingu na kupelekwa Uholanzi kusomewa mashitaka.

Najua mnapitia kipindi kigumu sana. Hivyo nawaelewa. Nazielewa fikra zenu tamanifu mlonazo.

Na ni fikra tu. Siyo uhalisia wala mwelekeo wa matukio ya kiuhalisia.
 
Ngoja waje jiandae kwa matusi, wapo wanaangalia EPL na VPL. Wote wanaoamini kuna mtu atapelekwa ICC ndo hao hao waliamini Lissu anaweza kuwa Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Huwa nawaita NYUMBU. Upeo wao wa kufikiri upo chini sana.
 
Nyani Marekani ni mmeba mabox huku kumbe ulirudi kusaidia kubeba mabox ya kura sa wizi kumsaidia Wanyumbani....
 
kwahio wasiposhitakiwa sisi itatusaidia nini? cha msingi kila mtu aendelee na mambo yake kuna njia nyingi za kudai haki sio lazima mahakamani hata kumlegeshea jambazi akampore au kumwua aliekudhulumu ni njia ya kisasi vile vile...kwahio usipate taabu kivile
 
kwahio wasiposhitakiwa sisi itatusaidia nini? cha msingi kila mtu aendelee na mambo yake kuna njia nyingi za kudai haki sio lazima mahakamani hata kumlegeshea jambazi akampore au kumwua aliekudhulumu ni njia ya kisasi vile vile...kwahio usipate taabu kivile
Punguza Jazba Kidogo,usifikie huko,hizi ni Siasa tu!!
 
Pinga pinga watakuja kupinga na hili. Wameshajazwa na shangazi yao huko twitani kwamba file limefika kwenye desk la ICC sasa hawaelewi kitu.
Hahahaa.

Ni bora wajikite kwenye kuelimisha watu kuhusu katiba mpya, tume huru ya uchaguzi, na kuhamasisha wananchi kuidai, kuliko kuwajaza matumaini hewa.
 
Back
Top Bottom