Fikra ya documentary: Historia ya Chama cha Makuli wa Dar es Salaam (Dar es Salaam Dockworkers' Union)

Fikra ya documentary: Historia ya Chama cha Makuli wa Dar es Salaam (Dar es Salaam Dockworkers' Union)

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
FIKRA YA DOCUMENTARY: DAR ES SALAAM DOCKWORKERS' UNION (CHAMA CHA MAKULI WA DAR ES SALAAM) 1947

Leo nimetembelewa na mwandishi kijana Charles Michael kutoka Morogoro.

Charles ni muhitimu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam ambako amesomea utengenezaji wa filamu na ni mwandishi wa BBC.

Alinipigia simu kutoka duka la vitabu la Ibn Hazm Msikiti wa Manyema ambako alinifahamisha kuwa amenunua kitabu cha Abdul Sykes na angependa tuonane kwa mazungumzo.

Tumeonana na amenieleza kuwa amesoma mtandaoni historia ya Dar es Salaam Dockworkers' Union kisa ambacho kipo katika kitabu cha Abdul Sykes.

Historia hii imempendeza sana kiasi ameamua kutengeza documentary yake na hiyo ndiyo sababu ya yeye kuja kuonana na mimi.

Kwa hakika kisa hiki kwa mara ya kwanza mimi nimekisoma kutoka kwa John Iliffe aliyekuwa mwalimu wa historia Chuo Kikuu Cha Afrika ya Mashariki, Campus ya Dar es Salaam katika miaka ya 1960.

Bahati mbaya mimi sikuwa nimeridhika na yeye alivyoeleza historia ya chama hiki kwa hiyo nikaamua kufanya utafiti wangu mwenyewe na niliyokuta katika utafiti huu ndiyo niliyoeleza katika kitabu cha Abdul Sykes.

Haya naamini ndiyo bila shaka yaliyomvutia huyu kijana Charles Michael kiasi kutaka kutengeneza documentary ya chama hiki.

Hiki ni kisa cha Waswahili wa Dar es Salaam vibarua wa bandari ya Dar es Salaam mwaka wa 1947 na kijana mdogo wa miaka 23 Abdul Sykes mtoto wa mwanasiasa na mfanya biashara maarufu Kleist Sykes.

Huu ni mkasa wa mwanasiasa maarufu wa nyakati zile Mkomunist Erika Fiah, Islam Barakat, Labour Inspector wa kwanza Mwafrika na G. Hamilton Mwingereza mtaalamu wa vyama vya wafanyakazi aliyeletwa Tanganyika mwaka wa 1948 kuisaidia Dar es Salaam Dockworkers; Union.

Mkasa unaanza Shambani kwa Mohamed Abeid, Bonde la Msimbazi vibarua hawa wa bandarini walipolishana kiapo kuamua kupambana na makampuni makubwa ya meli yaliyokuwa yanawanyonya kwa kuwapa ujira mdogo bila ya mkataba wowote.

Vibarua hawa walipata ushindi mkubwa katika mgomo wao na serikali iliwaruhusu kusajili chama na Abdul Sykes akachaguliwa kuwa General Secretary wa chama hicho kilichojulikana kama Dar es Salaam Dockworkers; Union mwaka wa 1948.

Kisa ni kirefu na kinaishia kwa damu kumwagika pale vibarua hawa walipofanya mgomo na kupambana na askari wa kuzuia fujo katika mitaa ya Dar es Salaam mwaka wa 1950.

Kisa hiki mimi binafsi kilinivutia sana mara ya kwanza nilipokisoma.

1643514562145.png
 
Back
Top Bottom