Fikra za kikoloni zina Waathiri wa Wakenya

Chamoto

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2007
Posts
8,577
Reaction score
18,774
Kabla ya mashindano makubwa ya mpira wa miguu kama UEFA au kombe la dunia kuanza, vyombo vya habari vya Uingeraza huongea sana kuhusu timu yao. Wakianza kuwasifia wachezaji wao utaamini kabisa kuwa mwaka huu hakuna timu itawafunga.

Na kwa kweli kama ushindi ungekuwa kwenye media basi Uingereza ingekuwa inashinda kila siku. Cha ajabu ni kuwa mashindano yakianza Uingereza huwa timu ya mwanzo mwanzo kutolewa.

Tabia hii ya Waingereza ya kujisifu sifu sana, kama mbwa anayebweka bweka bila meno imewaathiri sana wakenya. Kuanzia "koko" (babu) yao Njonjo mpaka vitukuu vyao sasa, ni kelele tuu wakati hamna kitu.

Utamkuta Mkenya anasema "sisi tuko na ghorofa mrefu East Afrika" wakati ukiliangalia jengo lenyewe unaona ni kiandunje fulani hivi kinachosaidiwa na Mnara.

Kwenye utalii watapiga kelele wakati mapato yao hata $1.4 billion hayafiki, kwenye uchumi watasema wana GDP kubwa huku watu wanakufa na njaa na ukiangalia "GDP to debt ratio" yao unaweza hata kupawa na ugonjwa wa moyo.

Kwenye jeshi ni hivyo hivyo kelele "mingi" lakini Alshabab wanakuja wanawachapa bakora na kuondoka bila wao kuwafanya kitu.

Jamani, ondokaneni na akili za wakoloni "wenyu" wenye kelele "mingi" kwa media lakini timu yao ni kichwa cha mwenda wa zimu Ulaya.

Mjitathmini ni wapi mnakosea kama nchi siyo kujitapatapa bila sababu, wenzenu ndo tunawaacha hivyo.
 
Kabla ya mashindano makubwa ya mpira wa miguu kama UEFA au kombe la dunia kuanza, vyombo vya habari vya Uingeraza huongea sana kuhusu timu yao. Wakianza kuwasifia wachezaji wao utaamini kabisa kuwa mwaka huu hakuna timu itawafunga.

Na kwa kweli kama ushindi ungekuwa kwenye media basi Uingereza ingekuwa inashinda kila siku. Cha ajabu ni kuwa mashindano yakianza Uingereza huwa timu ya mwanzo mwanzo kutolewa.

Tabia hii ya Waingereza ya kujisifu sifu sana, kama mbwa anayebweka bweka bila meno imewaadhiri sana wakenya. Kuanzia "koko" (babu) yao Njonjo mpaka vitukuu vyao sasa, ni kelele tuu wakati hamna kitu.

Utamkuta Mkenya anasema "sisi tuko na ghorofa mrefu East Afrika" wakati ukiliangalia jengo lenyewe unaona ni kiandunje fulani hivi kinachosaidiwa na Mnara.

Kwenye utalii watapiga kelele wakati mapato yao hata $1.4 billion hayafiki, kwenye uchumi watasema wana GDP kubwa huku watu wanakufa na njaa na ukiangalia "GDP to debt ratio" yao unaweza hata kupawa na ugonjwa wa moyo.

Kwenye jeshi ni hivyo hivyo kelele "mingi" lakini Alshabab wanakuja wanawachapa bakora na kuondoka bila wao kuwafanya kitu.

Jamani, ondokaneni na akili za wakoloni "wenyu" wenye kelele "mingi" kwa media lakini timu yao ni kichwa cha mwenda wa zimu Ulaya.

Mjitathmini ni wapi mnakosea kama nchi siyo kujitapatapa bila sababu, wenzenu ndo tunawaacha hivyo.
Sasa sisi tunawazidi nini watu wa Kenya kwa mfano.
1. Riadha na ndondi ktk national level wako mbele sana.
2. Viwanda tena ndiyo usiseme. Tanzania ni soko lao.
3. Mipira wa miguu na mikono ktk national teams wanatuzidi.
4. Democracy wanatuzidi mbali sana.
5. Huduma za afya & matibabu wako mbele kulinganisha na sisi.
6. Diaspora nje huko wanatutimulia vumbi
7. Mahakama zao angalau ziko vizuri kuliko zetu zinazoendeshwa ki siasa.

Sisi tunachowazidi Kenya ni ardhi kubwa, madini, vivutio vya utalii nk. Lakini napo hatuvitumii ipasavyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee, mafanikio ya wenzako yanakuuma kweli kweli, ugua pole. Unafananisha masuala ya kandanda na maendeleo ya nchi? Ila Kenya unayoiponda haitumii katiba iliyoandikwa na mkoloni kama nchi yako ya Tz, miaka zaidi ya hamsini baada ya kupata uhuru! Wala haitumii mifumo ya kikoloni kama ya miungu watu wenu maRC na maDC, wenye hulka za kikoloni. Tafakari hayo wakati unatazama uchanganuzi wa kandanda ya mkoloni wako mpendwa.
 
Navyojua bondia anayeshika nafasi ya juu Afrika ni Mtanzania, kwenye Afya tunaongoza kwenye kila sekta wakati Kenya inaomba msaada wa madaktari kutoka Cuba. Kuwa na Diaspora kubwa ni kiashiria cha kuwa na nchi yenye matatizo (watu wanaikimbia nchi yao). Demokrasia gani Kenya iliyonayo, wakati kati ya maraisi wanne, watatu ni Wakikuyu?
 
Aisee, mafanikio ya wenzako yanakuuma kweli kweli, ugua pole. Unafananisha masuala ya kandanda na maendeleo ya nchi? Ila Kenya unayoiponda haitumii katiba iliyoandikwa na mkoloni kama nchi yako ya Tz, miaka zaidi ya hamsini baada ya kupata uhuru! Wala haitumii mifumo ya kikoloni kama ya miungu watu wenu maRC na maDC, wenye hulka za kikoloni. Tafakari hayo wakati unatazama uchanganuzi wa kandanda ya mkoloni wako mpendwa.
Katiba ipi iliandikwa na mkoloni?
 
Sasa sisi tunawazidi nini watu wa Kenya kwa mfano.
1. Riadha na ndondi ktk national level wako mbele sana.
2. Viwanda tena ndiyo usiseme. Tanzania ni soko lao.
3. Mipira wa miguu na mikono ktk national teams wanatuzidi.
4. Democracy wanatuzidi mbali sana.
5. Huduma za afya & matibabu wako mbele kulinganisha na sisi.
6. Diaspora nje huko wanatutimulia vumbi
7. Mahakama zao angalau ziko vizuri kuliko zetu zinazoendeshwa ki siasa.

Sisi tunachowazidi Kenya ni ardhi kubwa, madini, vivutio vya utalii nk. Lakini napo hatuvitumii ipasavyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Number 2,3,4,5,7 hakuna eneo mkenya anaipita Tanzania hapo, wewe kama umekalia habari za ufipa 24/7 sio kama mambo mengine hayaendelei Tanzania

Tanzania imepiga hatua kwenye hizo sector kuliko nchi yoyote Africa mashariki na kati
 
Aisee, mafanikio ya wenzako yanakuuma kweli kweli, ugua pole. Unafananisha masuala ya kandanda na maendeleo ya nchi? Ila Kenya unayoiponda haitumii katiba iliyoandikwa na mkoloni kama nchi yako ya Tz, miaka zaidi ya hamsini baada ya kupata uhuru! Wala haitumii mifumo ya kikoloni kama ya miungu watu wenu maRC na maDC, wenye hulka za kikoloni. Tafakari hayo wakati unatazama uchanganuzi wa kandanda ya mkoloni wako mpendwa.
Mikoa, wilaya ni maneno tuu yanayomaanisha mfumo wa kiutawala, nenda hata Misri au Malaysia utaona wanatumia mifumo hiyo ya kiutawala n.k. Nyinyi kwa akili za kitumwa mnataka kuwa kama Wamarekani kutumia maneno kama senator sijui county, wapi na wapi?
 
Number 2,3,4,5,7 hakuna eneo mkenya anaipita Tanzania hapo, wewe kama umekalia habari za ufipa 24/7 sio kama mambo mengine hayaendelei Tanzania

Tanzania imepiga hatua kwenye hizo sector kuliko nchi yoyote Africa mashariki na kati
mmepiga hatua lakini bado hamjatufikia.
 
Mikoa, wilaya ni maneno tuu yanayomaanisha mfumo wa kiutawala, nenda hata Misri au Malaysia utaona wanatumia mifumo hiyo ya kiutawala n.k. Nyinyi kwa akili za kitumwa mnataka kuwa kama Wamarekani kutumia maneno kama senator sijui county, wapi na wapi?
Eti maneno tu, wenzenu wanawachagua viongozi wao. Wananchi wenyewe kwenye uchaguzi mkuu wakati nyinyi hapo maRC na maDC wanateuliwa na rais bila pingamizi kutoka kwa yeyote yule. Yaani bado unajivunia urithi wenu wa mifumo ya kikoloni miaka zaidi ya hamsini baada ya kupata uhuru?
 
Number 2,3,4,5,7 hakuna eneo mkenya anaipita Tanzania hapo, wewe kama umekalia habari za ufipa 24/7 sio kama mambo mengine hayaendelei Tanzania

Tanzania imepiga hatua kwenye hizo sector kuliko nchi yoyote Africa mashariki na kati
Ufipa nitoeko kabisa nazungumzia fact.
Angalau umekubali namba 1 na 6 tunazidiwa. Lakini hizo unazokataa fanya utafiti bila mhemuko wa kizalendo utakubaliana nami wako mbele yetu. Tufanye juhudi za makusudi kuwafikia ingawa na wanaendelea mbele. Mfano viwanda sisi tunafanya siasa kuwa viwanda 3000 vimeanzishwa ndani ya awamu ya 5, viko wapi ?!. Mfano mwingine ni mpira ukiondoa Azam, Simba na Yanga wenye wadhamini wa maana kulikobaki ni majanga pamoja na national teams .

Katika afya nimewahi kumrusha mgonjwa kwa ndege toka Mwz hadi Nairobi. Kila kipimo kilichotakiwa kilipatikana hata usiku wa manane mradi umelipa. Kwetu hapa ndiyo baadhi ya vipimo mh. Rais ameamuru vinunuliwe na bado vinapatikana ktk ngazi ya rufaa na si mikoani kuliko na wagonjwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Navyojua bondia anayeshika nafasi ya juu Afrika ni Mtanzania, kwenye Afya tunaongoza kwenye kila sekta wakati Kenya inaomba msaada wa madaktari kutoka Cuba. Kuwa na Diaspora kubwa ni kiashiria cha kuwa na nchi yenye matatizo (watu wanaikimbia nchi yao). Demokrasia gani Kenya iliyo nayo wakati kati ya maraisi wanne watatu ni wa kikuyu?

Machungu kweli.
Cuba na Kenya walifanya exchange programme. (knowledge transfer). Madaktari wa Kenya wako Cuba, wa Cuba wako Kenya.
Wote wanalipwa mishahara. Hakuna msaada.

Kama Tanzania inaongoza kwenye afya, kwa nini takwimu zinasema:
1. Mnaongoza kwa infant mortality
2. Nyinyi wa mwisho kwa life expectancy.
3. Nyinyi wa mwisho kwa health insurance coverage.
4. Nyinyi wa mwisho kwa doctor to population ratio.
5. 92% ya watoto wenu under 5 years wako malnourished.

Wewe unaelewa maana ya afya ni nini?
 
Eti maneno tu, wenzenu wanawachagua viongozi wao. Wananchi wenyewe kwenye uchaguzi mkuu wakati nyinyi hapo maRC na maDC wanateuliwa na rais bila pingamizi kutoka kwa yeyote yule. Yaani bado unajivunia urithi wenu wa mifumo ya kikoloni miaka zaidi ya hamsini baada ya kupata uhuru?
Huo ni utaratibu wetu tuliojiwekea hata hao wanaochaguliwa ni smoke screen tuu, tulio hapa tunaona kinacho endelea. Wengi wa hao masenator hasa republicans wanachaguliwa kimabavu kwa kutumia gerrymandering.
 
Machungu kweli.
Cuba na Kenya walifanya exchange programme. (knowledge transfer). Madaktari wa Kenya wako Cuba, wa Cuba wako Kenya.
Wote wanalipwa mishahara. Hakuna msaada.

Kama Tanzania inaongoza kwenye afya, kwa nini takwimu zinasema:
1. Mnaongoza kwa infant mortality
2. Nyinyi wa mwisho kwa life expectancy.
3. Nyinyi wa mwisho kwa health insurance coverage.
4. Nyinyi wa mwisho kwa doctor to population ratio.
5. 92% ya watoto wenu under 5 years wako malnourished.

Wewe unaelewa maana ya afya ni nini?

Hizo takwimu kila mtu anaweza kuzipika lakini tukiona wakenya wanakuja Tanzania kutibiwa kansa au kupasuliwa moyo, tunasena naam, sekta ya Afya imeimarika.
 
Navyojua bondia anayeshika nafasi ya juu Afrika ni Mtanzania, kwenye Afya tunaongoza kwenye kila sekta wakati Kenya inaomba msaada wa madaktari kutoka Cuba. Kuwa na Diaspora kubwa ni kiashiria cha kuwa na nchi yenye matatizo (watu wanaikimbia nchi yao). Demokrasia gani Kenya iliyo nayo wakati kati ya maraisi wanne watatu ni wa kikuyu?
Wewe kwani husomangi comments huku? Si ni juzi tu tumewaonyesha doctor to patient Ratio yenu ni kubwa mno kuiliko ya Kenya ama akili zako kama za ngiri?
 
Hizo takwimu kila mtu anaweza kuzipika lakini tukiona wakenya wanakuja Tanzania kutibiwa kansa au kupasuliwa moyo, tunasena naam, sekta ya Afya imeimarika.

Serikali ya udikteta wa Tanzania ina sifa dunia nzima kwa upishi wa data.

But here in Kenya you don't even have to take our word for it. Tunatumia data za mashirika ya kimataifa.
United Nations Conference on Trade and Development last year listed Kenya as one of Africa's top destination for medical tourism. Tanzania haipatikani popote kwenye hiyo list.

https://www.businessdailyafrica.com...al-tourism/3946234-4009460-smulr9z/index.html

Tanzania ambayo nchi nzima ya watu millioni 60 haina PET CT scanner, yaweza kuwa aje ndio destination ya wakenya kwa matibabu ya cancer? 😂😂😂
 
Back
Top Bottom