Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
‘’SISI NI WAYAHUDI’’ (THE BOY IN STRIPPED PYJAMAS)
Hiki ni kitabu kilichoandikwa na John Boyne na kikafanywa filamu.
Hii ni hadith katika mambo ya kweli kuhusu kijana wa miaka tisa Bruno ambae baba yake ni katika askari katika jeshi la Wajerumani wakati wa Vita Vya Pili Vya Dunia.
Baba yake ndiye kiongozi wa kambi ya mateso na mauaji ya Wayahudi.
Kisa kinaanza mara tu baada ya baba yake Bruno kuhamia kwenye kambi hiyo.
Mtoto Bruno anashangazwa na uzio wa miba ya chuma kati ya nyumba yao na kambi halikadhalika anashangazwa na watu na watoto anaowaona upande ule wa pili.
Ni watu kama baba yake na watoto ni watoto kama yeye lakini watu anaowaona upande wa pili wa uzio muda wote wako katika vikundi na wanaswagwa na wanaonekana wako katika majonzi.
Katika filamu kuna ‘’scene,’’ ya kumtoa mtazamaji machozi pale Bruno na rafiki yake wakiwa wametenganishwa na uzio wa miba ya chuma wanacheza ‘’draft."
Hili "draft" liko upande alioko Bruno.
Wayahudi ni hodari sana wa mambo haya wameweza kuhifadhi historia yao yote ya mateso katika mikono ya Manazi katika maandishi, sauti na picha na duniani pote utakapokwenda utakuta hizi makumbusho.
Turudi kwa Bruno na rafiki yake.
Muongozaji filamu hafanyi haraka kuondoa camera anataka mtazamaji ushibishe macho yako na anachokusudia kikuingie akilini.
Bruno amenawiri na kavaa nguo safi shati jeupe na kaptula iiyomkaa vema.
Rafiki yake kavaa pyjamas zilizochoka na zisizovutia kutazama na uso wake umesinyaa kwa shida.
Bruno akiwa pale katika mpaka ule anashuhudia mengi upande wa pili ambao hayaelewi na anamuuliza maswali rafiki yake.
Lakini katika maswali yote aliyomuuliza rafiki yake ambayo yeye hakuwa na majibu swali moja alikuwa na jibu lake.
Bruno alimuuliza, ‘’ Kwa nini nyinyi mko katika hali hii?
Rafiki yake alimjibu akamwambia, ‘’Sisi ni Wayahudi.’’