Johnny Sins
JF-Expert Member
- Nov 4, 2019
- 2,537
- 3,873
Kifo? Ndio, ipo app kwenye simu kwa ajili hiyo.
Ilianza kama utani, baada ya kujua kuna application inayotabiri binadamu umebakiza muda gani wa kuishi duniani. Marafiki wakaamua kuitumia kama mchezo ili ataebakiza muda mchache awanunulie wenzie pombe, hawakujua.
Walivotaka iwe mchezo na uishie pale pale bar, haikuwa hivo, na haukuwa mchezo tena ilikuwa ni baina ya kifo na uhai. Kila aliebakiza muda mchache alihitajika na umauti kwa njia asiyoitaka app haifutiki kwenye simu wala haizimiki.
Mmoja kati ya nesi wa hospitali ya jiji alipoamua kuucheza mchezo huo akiamini hauna ukweli ndipo alipojikuta anatakiwa kuyaokoa maisha yake na wote waliomzunguka.
Ni race against time, muda, ndio kitu pekee chenye maana kuliko vyote kwa nesi huyu, kadri app inavosoma kuwa muda unakwisha..ndivyo alivyotakiwa kuzuia kila analoona ni tishio kwake.
Hakuna kula, kunywa wala kulala. Unalalaje wakati simu yako inasoma muda kuja chini kuwa unakaribia kufa!..unakulaje ukiwa unafatwa na vitu vyenye kuogopesha. Hakuwa peke yake.
Kifo cha wengi si harusi! Basi walioipenda hiyo app walijulikana na wakaonana na wakashirikiana, ni vita baina ya binadamu na simu walizonunua wenyewe.
Ubaya ni kuwa hata ukiitupa ukaenda kununua mpya,ni ndani ya dakika moja ile app itakuja yenyewe, ni kizaazaa mjini.
Kwa wale wa movie za thriller na kutisha hii ndo mahala pake.
#COUNTDOWN..