Johnny Sins
JF-Expert Member
- Nov 4, 2019
- 2,537
- 3,873
Kwenye nyumba moja ya familia inayomilikiwa na mfanyabiashara maarufu panatokea mauaji ya kutisha na familia kuchomwa moto uliotokana na umeme, kwanini?
Muda hayo yanatokea upande mwingine kuna mtu anachinjwa hadharani na watu wasiojulikana,mbele ya umati wa watu,akiwa na begi mkononi, kwanini?
Na ndani ya muda huo pia askari anaezuia mwanamke asifanyiwe uhuni kwenye nyumba ya sinema. Askari yule anakufa mbele ya askari wenzie kifo chenye utata, kwanini?
Kwanini matukio haya yametokea kwa wakati mmoja,sehemu tofauti, kwanini?
Wakati polisi wanahaha kutafuta ukweli kwa kuunganisha matukio. Kitu ambacho hakihitaji akili ya kawaida inamtaka mtu anaefanya kazi kwa speed ya umeme. yeess!
.Ni detective kalyan, mwanasheria msomi kama kaka angu Msalaba Bernard anapelekewa kesi hii yenye utata, anaiuliza serikali mna bei gani? Serikali inamwambia saidia kutatua tatizo kwenye nchi yako, utapata heshima. Hapana kalyan hayupo hivo.
Yeye pesa mbele. Anapenda pesa pengine kuliko kitu chochote duniani. Labda ni kwa sababu anaamini uwezo wake ni katika kufikiria kwake jinsi ya kulivaa janga hilo ndipo anapopta jambo lingine dogo lenye ukubwa wake.
Mtoto wa miaka saba mwanafunzi,anamfata detective huku analia kuwa mbwa wake mdogo amekufa, amepigwa risasi, shida yake anamtaka aliemuua mbwa wake, serious?
Yaani kesi ya serikali hajaishughulikia,akaanze kutafuta mbwa. Yule mtoto alimpa hela zote alizokuwa anaweka kwenye kibubu chake akirudi shule, akamwambia ntaenda kumuibia baba angu hela nyingine nikupe unitafutie huyo mtu. Detective anacheka anamwambia sawa ntakutafutia.
Detective alitumia muda wake ambao kachoka kumtafutia dogo suluhu ya tatizo lake bila kujua kuwa kwa kutumia tatizo la dogo ndipo kwenye kiini cha matatizo yote yaliyoikumba nchi, hujaelewa? Ni hivi, kesi ya mbwa wa dogo ndio imeamua mechi.
Mfano mtu anaetumia mkono wa kushoto anajiua vipi kwa kujipiga risasi kwa kutumia mkono wa kulia? Moja kati ya idea za kibabe sana, inayopelekea taharuki ya nchi na wakubwa wasijue wafanye nini.
Detective kila alipokuwa anakaribia kuupata ukweli wa mbwa wa dogo ndivo alivogundua mambo makubwa yaliyotokea kwa kupangwa kiufundi na watu wenye akili za kutosha sana.
Mwanaume akaingia kazini kwa kesi ya mbwa. Kila alipopata kujua hili ndipo password ya kila kwanini ilipofunguka ni tishio la nchi lililomalizwa kwa kesi ya mbwa.
Detective ameipata heshima ya nchi kwa shilingi elfu mbili tu ya dogo.
#DETECTIVE....