Filamu ya IT

Filamu ya IT

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
Ninachompendea Stephen King ni ule uwezo wake wa kuandika visa tetemeshi sana kutokana na wazo la kawaida mno - wazo ambalo mara nyingi watu hawalifikirii mpaka walisome kutoka kwake.

Sasa kwenye kitabu chake alichokiita "IT" kilichouzwa nakala nyingi sana duniani na kutengenezwa filamu angalau mara mbili mpaka sasa, Stephen King analiongelea “JITU”, ambalo ndilo wahusika wa kisa cha kwenye kitabu hiki waliliita IT( siyo I.T. ya Information Technology!!), bali “it” ya li-JITU lisilo binaadamu.

Hili JITU kimsingi ni zimwi lenye sura ya “clown”- ambapo kule kwa wenzetu, “clown” ni rafiki wa watoto - akiwachekesha kwenye mabembea na kuwapa zawadi mbali mbali hususan maputo. Lakini hili “IT” la kwenye kisa hiki lililojivisha sura ya rafiki wa watoto, ni zimwi lenye njaa, uwezo wa kimazingaombwe na nguvu za ajabu. Lenyewe hutafuna watoto bila huruma na kuua watu kinyama kwa nguvu zake za kiajabu-ajabu; huku likijidhihirisha kuwa ni jitu lisilowezekana na lenye kuogopesha sana.

Basi JITU hili lilikuwa likiibuka kwenye mji mdogo wa Derry kila baada ya miaka 27 na kufanya mauaji yake kisha linapotea. Na kisa kinapoanza, JITU linamtafuna na kumpoteza kabisa mtoto wa miaka mitano. Kaka wa mtoto aliyetafunwa na JITU, ambaye wakati huo alikuwa ana umri wa kama miaka kumi hivi, akishirikiana na wenzake sita wenye rika kama lake wanaazimia kulifuatilia na kuliangamiza lile JITU pindi litakaporudi tena baada ya miaka hiyo 27, wakati huo na wao watakuwa wameshakuwa watu wazima.

Na kweli, miaka 27 baadaye JITU linarudi tena Derry. Na wale watoto ambao sasa ni watu wazima wanaitana kila moja kutoka kwenye mji aliohamia, na kurudi Derry kuja kulikabili na kulipiza kisasi. Hapo wanafanikiwa kumuokoa mtoto mwingine aliyekuwa anakaribia kutafunwa na JITU. Nalo linawakasirikia sana, nao wanapambana nalo vikali. Ndipo wanapogundua siri ya nguvu za ajabu za lile JITU - na hapa ndipo Stephen King anaponikosha.

Wanagundua kwamba "It feeds on your fears."

Yaani kumbe kadiri unavyoliogopa na kujawa na woga dhidi yake, ndivyo lile jitu linavyozidi kupata nguvu na ule uwezo wake wa kimiujiza wa kukutisha na kukuangamiza. Kwamba woga wa binadamu dhidi yake ndio chakula chake.
Unaona?

Wazo la kawaida mno, lakini pia, lililo tata sana.

It feeds on your fear!

Twaba’an! Wale wahusika wakuu walipoigundua siri hii, wakalitunishia JITU kifua. Wakalishambulia kwa maneno makali sana, wakiliambia kuwa HAWALIOGOPI, na wala HALIWATISHI.

Maneno haya “sikuogopi”, “hunitishi”, “wewe muoga tu, ndio maana unawashambulia watoto wadogo tu miaka yote”, yalikuwa kama risasi za moto kwa lile JITU linalopenda mno “chakula” cha kuogopwa.

Nalo likajitahidi kupambana. Likazidi kuwaungurumia na kuwatisha kwa vitimbi lukuki, huku likijibadilisha sura na maumbile kadhaa ya kutisha; lakini kila lilivyozidi kuwatisha kwa mazingaombwe yake ya kiza, ndivyo na wao walivyozidi kulibishia kuwa hawatishiki nalo - na kadiri walivyozidi kulibishia namna hiyo, ndivyo zile nguvu zake za ajabu zilivyokuwa zikipukutika.

Hatimaye lenyewe ndio likawa limejaa woga baada ya kukosa “chakula”, ambacho ni woga lililoutarajia kutoka kwa wale liliowakusudia wawe wahanga wake.

Mwisho likaangamia mithili ya puto lililowamba na kudungwa mwiba mkali - kwa woga mkubwa na idhilali kali.
Waliosoma na watakaosoma kitabu hiki hakika watakuwa wamepata mazingatio makubwa sana ikiwa watakuwa ni wenye kutafakari.

Kwani hata na kwenye maisha yetu ya kila siku watu wa namna hii tunao - watu ambao chakula chao ni kuona au kutengeneza madhila ya namna fulani kwa wengine.

Watu makini huamua kuwaacha wafe kwa njaa.
Ndimi hapa.
HIT.
21.05.2020



Credit: Hussein Tuwa
 
MTUNZI HUSEIN TUWA HAJAWAHI KUNIANGUSHA KATIKA RIWAYA ZAKE, HUTUMIA AKILI NYINGI MNO.
SIO WALE WAZEE WA KUTUNGA HADITHI SIJUI MTU AKAZIMIA MIAKA 20, MATUKIO YALE YALE ANABADILI TU MAJINA YA WAHUSIKA
 
Kwahiyo tunaweza kulifananisha na covid19? Kwamba ukiigopa Ndio inazidi kuua ila dingi kaitunishia kifua kuwa hatuiogopi na imeanza kunywea?
 
Back
Top Bottom