Filamu ya Kiswahili, Jina la Kiingereza....

Filamu ya Kiswahili, Jina la Kiingereza....

Nyundo_tz

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2009
Posts
640
Reaction score
20
Wadau, soko la filamu linakuwa kila siku hapa nyumbani. Lakini je, kuna ulazima wa watengeneza filamu hizi kuziita majina ya Kiingereza ili hali ndani wanazungumza kiswahili mwanzo mpaka mwisho?
 
Ulimbukeni wa kutupwa...Wanadahani kwa kufanya hivyo watauza zaidi, na kuonekana wajuvi wa mambo!
 
Ulimbukeni wa kutupwa...Wanadahani kwa kufanya hivyo watauza zaidi, na kuonekana wajuvi wa mambo!
Tatizo kubwa la wasanii wetu wakishaambiwa kwamba wana vipaji wanakuwa na imani kwamba vipaji vyao vitafafanya kila kitu kitu ambacho kwa akili ya kawaida tu hakiwezekani. Ki msingi wanatakiwa wawe na washauri (mameneja ambao watawashauri ki taaluma na kimasoko kwamba kipi ni sahihi kufanyika na wakati gani.
 
Toa mifano ya filamu hizo.

Diversion of love, dangerous desire, fake pastors, village pastors, yellow banana - hii sijui ilimaanisha nini coz yaliyomo ni tofauti na title yenyewe... Nafikiri mbonea ataje nyengine...
 
hakuna ulazima hata kidogo ...ila na mie nishangae kama wewe
 
Wasaniii wetu wote njaa kali na waganga njaa, what they are doing is coping Naija movies kwa kila kitu, hawana elimu ya cinema, wanachofanya ni maigizo, ila kwa sababu soko lao ni la uswazi wacha wawe macelebrity
 
Toa mifano ya filamu hizo.
Wala hakuna haja ya mifano,ni kitu ambacho kiko dhahiri...Karibu kila filamu ya Kibongo ina jina la Kiingereza...Karibu 90% kama sio 95% ya filamu za Kibongo zina majina ya Kiingereza..Ni ulimbukeni tu na kutokujiamini pamoja na kukalia kuiga filamu za wapopo(WaNigeria) kunakofanywa na waigizaji na Wazalishaji wa Kibongo ndo kuapelekea kuwpo kwa upuuzi huu...Jamaa wanakandamiza9wanaiga) sana kwa waNigeria....Mpaka inakera na kutia kinyaa
 
Filamu ina title ya Kiingereza, waigizaji wanaongea kiswahili. Aibu ni pale kiswahili kinachoongelewa kinapotafsiriwa......mf. Tafuna eti inatafsiriwa Cut...aibu, hivi hakuna washauri au baraza la filamu haliyaoni haya makosa.
 
Ukiangalia hizo sub-titles ndio utazimia kabisa!
 
wameniacha hoi na kuja na This is It! huh jamani ...............mpaka kitu kama hicho lazima tu copy?!
 
mwanzo mpaka MWISO?
Wadau, soko la filamu linakuwa kila siku hapa nyumbani. Lakini je, kuna ulazima wa watengeneza filamu hizi kuziita majina ya Kiingereza ili hali ndani wanazungumza kiswahili mwanzo mpaka mwiso?
 
Ukiangalia hizo sub-titles ndio utazimia kabisa!

yaaani mwalimu hapo ndo kwisha habari yake kabisaaaaa

btw wewe mwalimu si unaweza kuwasaidia kwenye hili janga?! (mwenzio wa kipeuo cha pili si unamwona?)
 
Back
Top Bottom