Zion Daughter
JF-Expert Member
- Jul 9, 2009
- 8,921
- 4,240
Mkuu acha masihara.
Zaidi ya asilimia 90 ya filamu za kibongo ni majina ya kizungu.
Wadau, soko la filamu linakuwa kila siku hapa nyumbani. Lakini je, kuna ulazima wa watengeneza filamu hizi kuziita majina ya Kiingereza ili hali ndani wanazungumza kiswahili mwanzo mpaka mwisho?
Naamini katika baadhi ya filamu wanachanganya lugha (Kiswahili na Kiingereza). Hiyo inaonyesha bidii ya kutaka kuitangaza zaidi filamu ieleweke kwa wasiojua kiswahili na pia inawasaidia kupata experience kuongea kiingereza. Jamani wanajitahidi, kwani mwanzo hawakuwa hivi. Filamu zao nyingi hivi sasa zinaburudisha. Kidogo kidogo watapiga hatua. Ila michango kama hii ya kuboresha zaidi filamu zao ni muhimu.
Hongereni sana The Great na The Greatest!
my dreams,this is it,one by one.......halafu majina yenyewe ni direct translation
Mkuu acha masihara.
Zaidi ya asilimia 90 ya filamu za kibongo ni majina ya kizungu.
Girl friend, Best friend, In the house na Lovely Gamble inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni kwa mujibu wa Asha Baraka wa ASETToa mifano ya filamu hizo.
Diversion of love, dangerous desire, fake pastors, village pastors, yellow banana - hii sijui ilimaanisha nini coz yaliyomo ni tofauti na title yenyewe... Nafikiri mbonea ataje nyengine...
Girl friend, Best friend, In the house na Lovely Gamble inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni kwa mujibu wa Asha Baraka wa ASET
Filamu ina title ya Kiingereza, waigizaji wanaongea kiswahili. Aibu ni pale kiswahili kinachoongelewa kinapotafsiriwa......mf. Tafuna eti inatafsiriwa Cut...aibu, hivi hakuna washauri au baraza la filamu haliyaoni haya makosa.