Filamu ya Mapanki - Darwin's Nightmare

Filamu ya Mapanki - Darwin's Nightmare

Teknocrat

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2018
Posts
4,967
Reaction score
11,056
Baada ya kuona Yule muuza silaha haramu nguli duniani Victor Bout ameachiwa na US, nikakumbuka ile docudrama ya Darwins Nightmare, filamu ya mapanki.

Ikabidi niitafute upya niiangalie baada ya miaka zaidi ya kumi.

Hivi wazee Mwanza , tupeni basi historia fupi ya kipindi kile, Mwanza kujishtukia ghafla na kuwa kati busiest Airport in East Africa nzima, kwa ili midude ya kirussia ilikuwa inatua pale ..Ilyushin II-76.

Kipindi kile maisha yaliwaje Mwanza , je mzunguko wa pese uliongezeka kulingana na sasa?

Na pia baada ya ile filamu kutembea nchi ulaya, nasikia wazungu wakapiga marufuku samaki wa sangara kwenye nchi zao, na kupelekea kushuka kwa soko la kimataifa. Kuharibia maisha ya watu Mwanza ambao walikuwa wanajishulisha kwenye biashara ya minofu ya sangara.

Je kulikuwa na athari za kiuchumi kwa mkoa wa Mwanza baada ile filamu?

Pia Jakaya, alilaani sana ule upotofu ulio unyeshwa akaanzisha ampeni. Ambayo ikapata sapoti ya wanahabari nguli duniani na wakaanzza kumshabulia yule muuandaji wa hii filamu kwa upotofu ulionyeshwa na kuleta taswira mbaya nchini.

Pia nasikia wale waliokuwa wanaonyeshwa kwenye hiyo filamu, walikuja kupewa kashkash na mapolisi kichizi na mpaka yule mwandishi aliyeunganisha doti za ndenge zinaleta silaha zitua na kupakia samaki zikiondoka, je ni kweli?
Tunawaomba mtupe ukweli kutoka nyie wenyewe wazawa wa Mwanza ?
 
Yule jamaa alinunua kampuni flani ya ndege ya uganda ndio akawa anaitumia safirisha silaha ilipostukiwa akawa anatunia kampuni ya ndege ya mke wa general Saleh, sijui ni ndugu au mtoto wa mseven mkewe huyo saleh anamiliki kampuni ya ndege ndio ikawa inaisaidia kampuni ya huyo jamaa kusubmit flight plan.

Inadaiwa jama alikuwa so much connected na utawala wa uganda na rwanda na congo na alikuwa ana machimbo ya almasi huko congo
 
Yule jamaa alinunua kampuni flani ya ndege ya uganda ndio akawa anaitumia safirisha silaha ilipostukiwa akawa anatunia kampuni ya ndege ya mke wa general Saleh, sijui ni ndugu au
Nimejaribu kutafuta sana hii habari ya filamu ya mapanki kupata ukweli wa waakazi wa Mwanza.

sikuona kitu zaidi ya Taarifa ya uchunguzi uliofanya na mamlaka ya usafiri wa anga kuhusu ndege mojawapo iliyoanguka...
 

Attachments

Kuna yule kijana mchoraji, alikuwa na jitahidi kujieleza, kuna wakati alisema kuwa moja ndege iliwahi kukamatwa na silaha na hii habari ilikuwa kwenye vyombo vya habari Tanzania , je ni kweli?

Japo baadae ilikuja kugundulika yule muuandaaji, alikuwa anawalipa hela ili waiigize anavyotaka, baada ya uchambuzi uliochakachuliwa na baadhi ya waandishi wa habari wa nchi tofauti duniani kuona alikuwa na dhamira ya kuharibu taswira yote pamoja na biashara ya minofu ya samaki.

Kwa kuwa aliiona inaiingilia na uuzaji wa silaha harumu ambazo zilikuwa zinaenda Congo DRC, au alikuwa na nia ya kujaribu kuongelea biashara ya silaha, lakini ili apate urahisi wa kibali cha kutengeneza hio filamu, akaaingiza biashara ya minofu ya samaki kama cover stori, bila yeye kujua athari iliyoleta kwa wananchi wa Mwanza kwa kuharibu biashara ya minofu ya sangara.

Na pia hata jina la filamu, lilichakachuliwa na lilikusudiwa ili kujenga mzuka kwa wazungu kuwa na shauku ya kujua hii filamu inahusu nini...

Pia kuingiza maisha ya watoto wa mtaani na madada poa, ilileta maswali mengi kwa nia yake ya hii filamu.

Japo kulikuwa na ukweli fulani labda kwenye biashara ya silaha, maana sio kwa mindege ile na kasi ya kuingia na kutua iliyoamsha shamrashamra katika mji wa Mwanza...
 
Ina maana hakuna hata msukuma mwenzangu aliyekuwepo kile kipindi cha filamu ya mapanki na ndege za kirussia...
Hata yule mchoraji haijui JF.....na kiingereza chake kizuri tu sana....na mwenye charitable heart....
Hata yule mlinzi anayefanya kazi Fish Reseaech Institute kama alivyosema, anaonekana kama ni Mkurya, ambaye hakuvumilia upumbavu wa Sir Meja na na amri za kipuuzi jeshini huku ana upinde na mikuki, anaongea kiingereza si haba na mwenye akili ya kupambana na mwizi kama yuko vitani na pia kutaka vita nyingine itokee ili aitwe tena jeshini apate nafasi nyingine ya kurudishwa jeshini....na yeye pia haijui JF....
Na yule mwalimu mstaafu.....na aliyesema Poverty is vicious cycle, if you are born with poor parent , you will end up poor and even if you bring your kids in this life will end up poor like yourself......alitisha sana...na yeye pia haijui JF aje kutuelezea zile zama....

Basi JF kwishnei kwa sisi wahenga....
 
'…omba omba wapo Dunia nzima …hata Kyle Newyork nikitoka Dukani huwa nakuta ombaomba wa kizungu wakiomba 'keep change'…' JK 2007


miaka ile hapakuwa na chawa kama leo wa kutolea ufafanuzi
 
Back
Top Bottom