Johnny Sins
JF-Expert Member
- Nov 4, 2019
- 2,537
- 3,873
Walimaliza kupendana kwa simu, wakawashirikisha wazee mapenzi yao. Kupanga tarehe haikuwa kazi, misingi ya harusi ikaandaliwa, ioni moja tulivu wawili hawa wakafunga ndoa, ikawa rahisi tu.
Grace msichana asieamini kwenye pesa aliwekeza moyo wake kwenye mapenzi zaidi. Alimpenda kijana wa nyumba hii na alitaka kuishi kama mke, ndani ya himaya ya kifalme.
Le Domas Fortune, nyumba ya kitajiri yenye watu matajiri, vyumba zaidi ya 130. Kila kitu ndani, heshima ya utawala na walinzi wa kila aina. Wafanyakazi wasio na idadi. Grace akajua maisha kayapatia. Maskini, alikosea kuamini!
Utajiri wa ufalme huu umetokana na uchezaji wa kamari. Numba nzima ina mila na desturi za kuamini kuwa kamari ndo asili ya utajiri wao. Na ataeoa au kuolewa nyumba hii atatakiwa kucheza mchezo unaohusisha kamari ama mila ya kumkaribisha mgeni ndani. Utachagua karata na utafanya kilichoandikwa kwenye karata hiyo. Ni karata ndo iliyoibua kizaazaa.
Grace alichagua kadi itayomtaka acheze "hide and seek" (kujificha ukitafutwa) akacheka akijua ni mchezo rahisi utaoleta furaha ndani ya nyumba yake mpya.Haikuwa hivo.
Muwewe aliumia sana alivyoona mkewe kachagua kadi ile sababu yeye anajua kitachotokea na hakutakiwa kumwambia mkewe kabla, ni kanuni na mila na desturi za utajiri wao. Mchezo ukaanza, Grace akaenda kujificha.
Hakukutakiwa ifike asubuhi Grace alitakiwa apatikane na auwawe. Nyumba nzima ilimsaka kwa kila aina ya silaha, na aliposhuhudia risasi ikimpasua kichwa mfanyakazi wa ndani badala yake, akagundua sio mchezo tena, ni vita.
Alitakiwa awe shujaa wa maisha yake mwenyewe ndani ya masaa 12 kuitafuta alfajiri. Ikifika alfajiri hajafa basi kafanikiwa, na kuifikia asubuhi haikuwa rahisi.
Usiku wa kwanza wa ndoa ndio usiku wa kwanza wa kukiona kifo chake hadharani. Bi harusi akachana shera akaingia stoo akatoka na silaha za kivita, ilikuwa hakuna namna.
Ni mauaji na vita visivomuhusu jirani. Mumewe alipoamua kumsaidia mkewe sababu ya kumpenda, vita ilihamia kwake, walitafutwa ye na mkewe, kanuni ziliwabana.
Ni asubuhi ifike au ufe kabla ya jua kuchomoza.
Credt: Kaisal Ally