Filamu za Kimkakati Kuandaliwa Kuelezea Utamaduni na Vivutio vya Tanzania

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

FILAMU ZA KIMKAKATI KUANDALIWA KUELEZEA UTAMADUNI NA VIVUTIO VYA TANZANIA

Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia Bodi ya Filamu @tanzania_film_board na Michezo ya Kuigiza imeandaa Mkakati madhubuti wa kuandaa Filamu tano ambazo zitaelezea utamaduni, vivutio vya ndani, historia na kuhamasisha uzalendo na utaifa kwa vizazi vijavyo.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Oktoba 23, 2024 Bungeni Jijini Dodoma wakati akiwasilisha taarifa kuhusu Mikakati madhubuti ya kukuza Sanaa nchini hususani tasnia ya Filamu, kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo chini ya Mwenyekiti Mhe. Husna Sekiboko.

Mhe. Ndumbaro amezitaja Filamu hizo kuwa ni Filamu ya Chifu Kingalu, Filamu ya Asante, Filamu ya Mwalimu Nyerere na Tamthilia inayohusu masuala ya Bima na Filamu ya A Trip With Your Wife, lengo likiwa ni kuitangaza Tanzania katika nyanja mbalimbali kupitia Filamu na kuwatafutia soko wadau wa filamu nje ya Tanzania.

"Kwa sasa Bodi inakamilisha Mkakati wa kuunganisha Mfumo wa kidigiti wa (Arts Management Information System - AMIS) na mifumo mengine ya TAUSI kutoka TAMISEMI, COSOTA NIDA, BRELA na TRA ili kiwafikia wadau bila kuwa na haja ya kufika ofisi za Bodi kupata huduma" amesema Mhe. Ndumbaro.

Wakichangia taarifa hiyo, Wajumbe wa Kamati wameelekeza wizara kupitia Bodi ya Filamu, kutengeneza mpango mahususi wa kuunga mkono uandaaji na usambazaji wa Filamu za Tanzania pamoja na kuwafikia wasanii walioko vijijini.
 
Attachments

  • GakGUM4XIAA21Sg.jpg
    GakGUM4XIAA21Sg.jpg
    235.6 KB · Views: 8
  • GakGUQ6WcAAwLpC.jpg
    GakGUQ6WcAAwLpC.jpg
    406.8 KB · Views: 3
  • GakGUQ4WIAApC85.jpg
    GakGUQ4WIAApC85.jpg
    267.3 KB · Views: 5
  • GakGUTBXwAAwT_t.jpg
    GakGUTBXwAAwT_t.jpg
    397.5 KB · Views: 3
  • Screenshot 2024-10-23 at 18-19-38 Wizara ya Sanaa(MCAS) (@wizara_sanaatz) • Instagram photos a...png
    Screenshot 2024-10-23 at 18-19-38 Wizara ya Sanaa(MCAS) (@wizara_sanaatz) • Instagram photos a...png
    890.1 KB · Views: 5
Nilishaandaa Script ambayo sio tu itamulika urithi wa tamaduni zetu , vivutio vya asili na kuenzi maono ya viongozi mashujaa wetu waliopita bali Nina uhakika haki ya Mungu hii script itafanya mapinduzi kwenye sekta ya elimu.

Kuna kizazi nitaki influence kupenda Shule na maarifa kuliko starehe za hovyo. Shida Sasa ntaupeleka wapi huu mzigo wa mawazo tu bila kuwa na pesa...
Kila sehemu Zina watu wao, tunakufa na vipaji na michango yetu ambayo ingeibadili jamii yetu maskini kuwa matajiri bila kuwaza u freemason, uchawa na mauaji ya albino (Roho imepata uchungu) .......... Asanteni
 
FILAMU ZA KIMKAKATI KUANDALIWA KUELEZEA UTAMADUNI NA VIVUTIO VYA TANZANIA

Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia Bodi ya Filamu @tanzania_film_board na Michezo ya Kuigiza imeandaa Mkakati madhubuti wa kuandaa Filamu tano ambazo zitaelezea utamaduni, vivutio vya ndani, historia na kuhamasisha uzalendo na utaifa kwa vizazi vijavyo.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Oktoba 23, 2024 Bungeni Jijini Dodoma wakati akiwasilisha taarifa kuhusu Mikakati madhubuti ya kukuza Sanaa nchini hususani tasnia ya Filamu, kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo chini ya Mwenyekiti Mhe. Husna Sekiboko.

Mhe. Ndumbaro amezitaja Filamu hizo kuwa ni Filamu ya Chifu Kingalu, Filamu ya Asante, Filamu ya Mwalimu Nyerere na Tamthilia inayohusu masuala ya Bima na Filamu ya A Trip With Your Wife, lengo likiwa ni kuitangaza Tanzania katika nyanja mbalimbali kupitia Filamu na kuwatafutia soko wadau wa filamu nje ya Tanzania.

"Kwa sasa Bodi inakamilisha Mkakati wa kuunganisha Mfumo wa kidigiti wa (Arts Management Information System - AMIS) na mifumo mengine ya TAUSI kutoka TAMISEMI, COSOTA NIDA, BRELA na TRA ili kiwafikia wadau bila kuwa na haja ya kufika ofisi za Bodi kupata huduma" amesema Mhe. Ndumbaro.

Wakichangia taarifa hiyo, Wajumbe wa Kamati wameelekeza wizara kupitia Bodi ya Filamu, kutengeneza mpango mahususi wa kuunga mkono uandaaji na usambazaji wa Filamu za Tanzania pamoja na kuwafikia wasanii walioko vijijini.
Filamu zinazohusu utalii huwa haziandaliwi na serikali na vyama dola, zikiandaliwa hivyo hupoteza lengo kwa kujikita kwenye siasa.
Tanzania bado hatujafikia kiwango cha kutengeneza filamu.
 
Sahihi kabisa. Hizo filamu ni upotevu wa pesa tu za walipa kodi na ni aina nyingine ya ubadhilifu wa mali za umma. Filamu hazitengenezwi hivyo wanavyojaribu kufanya.

Filamu kama ya Mwalimu Nyerere hauwezi kuifanya katika fungu la filamu kama hivi, utaishia kutoa kituko tu. Ni kumkosea heshima.
 
Back
Top Bottom