Filamu zetu zifikie kiwango cha juu Kimataifa

Filamu zetu zifikie kiwango cha juu Kimataifa

Askarimtu

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2019
Posts
277
Reaction score
185
Nimechoka sana na nasikia aibu jumlisha wivu , kuangalia filamu za wenzetu zikiendelea kukosha nyoyo zetu hasa kipindi hiki cha Mzee barakoa.

Inabidi watu waibuke wasapoti kazi za sanaa yetu kama tulivofanikiwa katika nyanja ya uongozi bora (nitabishiwa hapa), vipaji kichwani (kiakili), na sasa katika sanaa ya mziki. Ngoja nikudadavulie kidogo niliyoyataja:

1/ Watanzania ni watu waliobarikiwa sana japo wengi hawajui. Tuna historia kubwa sana katika uongozi bora, utulivu na ujasiri. Mfano: Hakuna mtu msomi duniani (active)asiyejua kuhusu Mwl. JK Nyerere. Nyuma yake kuna viongozi kibao ambao bado ni hazina ya nchi, japo hao viongozi bado hawakubaliwi na watu wote kama ni viongozi bora.

2/ Watanzania hasa katika vipaji kiakili ni watu ambao wanapenda ushindani na ubora ila baada ya hapo vipaji hufa kwa kutoendelezwa. Mfano mdogo tu; Katika vyuo vya kimataifa watanzania husifika kwa kuongoza kwa kupata alama za juu kabisa. Ni ngumu kushindana na mtanzania akiamua kupiga msuli. Wengi waliosoma nje ya nchi wanakubaliana na hii.

3/ Achana na hazina ya nchi katika maliasili, njoo tu kwa sanaa ya nchi hasa muziki. Muziki wa tanzania kwa sasa upo katika PEAK, maana hakuna mtu duniani asiyeupenda. Mwaka fulani nilishangaa sana kuona mwarabu anampenda shilole, siku haianzi bila kumsikiliza shilole. Now kuna Nandy, Diamond , Kiba na wengineo ambao miziki yao ndio inaua miziki ya nchi nyingine. Hakika hakika nakwambia watu wanaimba kiswahili japo hawaelewi maana yake...

SASA, tatizo naona hatuna stori nzuri ambazo zitateka soko la filamu lifike mbali zaidi.....

Siku hizi nimeacha kuangalia filamu za kizungu kwasababu ya tabia zao za kishoga na mambo kama hayo, ila nikiangalia basi ujue kuna meseji naifuatilia, mfano; movie ya venom (2018), nimeiangalia kwa sababu tu nilisikia wazungu wanataka kuanzisha aina mpya ya binadamu kwa kufanya merge kwenye DNA za binadamu na za viumbe vya ajabu. Lakini nilipokuja kuangalia drama za Asia ndipo hapo nikasikitika sana, hasa wakorea na wachina. Nimeangalia nyingi mno mpaka nimejua historia za hizi nchi mbili (hasa napenda historical dramas).

Lakini kwa nini tanzania hatujawahi kuigiza vitu kama hizi za mapanga mapanga?? mavisu visu, mamshale?? Je, machifu zetu walikuwa hawapigani na hivi vitu?? Rise and Fall of Songhai Empire inasaidiaje watu kuinua sanaa na uchumi wa nchi?? Jamani hata hakuna series ya MajiMaji war?? Au unataka mzungu aje aigize apige hela, halafu baadae tujilaumu?? Yaani hata stori kama za Tarzan hatuna,wakati wanyama wako kwetu?? Nasikia kule mikoani kuna stori nyingi za kufikirika za mababu zetu ambazo huwezi kuzipata darasani, inamaana hakuna watu wa research kwenda kuchukua hizo stori na kuzicheza?? Shida ni nini sasa?? WEWE, najua utasema shida pesa na vifaa.

Hivi kuandaa project ya bilioni 1 ili upate bilion 5 HAIWEZEKANI?? au ni kosa?? Au hakuna mtunga/mtafutaji stori?? Tubebe soko la Afrika hapo pia ili nchi ipae kwenye nchi ya viwanda vya movies pia.

Msipoigiza hizi drama nitapiga hela mwenyewe baada ya miaka 3 ijayo, ngoja niwauzie vijimifano kwanza hivi vichwa vya habari kwa wapika stori;

1/ Ethiopia kuna stori kuwa sanduku la agano lilifichwa Kilimanjaro na Mfalme Suleimani wakati Kenya linadaiwa lipo chini ya wakikuyu.
2/ Yule malkia wa mkoa fulani aliowakimbiza wajerumani na nyuki.(wakina mzee msisiri pamoja na yule bibi mwenda 😀, najua umenipata... )
3/ Hata stori ya utumwa tu kama Kunta kinte.
4/ Ile stori ya jitu kubwa kule tanga na bagamoyo.
5/ Popo bawa je? (natania tu), ila kiukweli hatujui lilikuwa jini au ni mtu au lilikuwa kafara linalipiza kisasi.
6/ Vita vya mkwawa na ndugu wake, mpaka kuja kuwashinda wajerumani. Yaani hapo stori inaandaliwa kuanzia baba ake mkwawa anavogawa urithi kwa wanawe mpaka chuki inavotokea, mpaka mmoja anavyomshinda mwenzie.
7/ Rhapta. (Nina uhakika hujui maana ya hili neno). Katafute maana yake maana ni historia yetu.

******************************************************************************************************************************
Kumbuka Barakoa,
S.L.P Covid-19,
CoRoNa City.

Dear filamu,

Usiniulize kama nimefikiria hivo, kwanini nisingetekelezaga mapema mawazo hayo. Tafadhali jijibu mwenyewe.

Wako mtiifu,

AKILI ZA KARANTINI.
 
ktk kila kazi inayofanyika kuna mtu analalamika na ktk kila kazi kuna mtu amefanikiwa kwahiyo kila kazi inahitaji mtu sahihi wa kuifanya.

Sent from my SM-G975F using Tapatalk
 
Nimeipenda hiyo ya popobawa, ingekuwa scary movie nzuri tu ya kibongo.
Watunzi wako wengi sana hata humu jf kuna story za watu ukizisoma ni script tosha. Nadhani shida ipo kwenye taasisi yenyewe ya filamu(bongomovie) hawajui wanafanya nn.

Kuna story za watu humu ukisoma unaweza tengeneza series nzuri tuu shida sisi wengine sio wasanii, mfano kuna dada alikuwaga anajiita Lara1, hadithi zake zingeweza kuwa kaseries flani ka madada wa mjini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeipenda hiyo ya popobawa, ingekuwa scary movie nzuri tuu ya kibongo.
Watunzi wako wengi sana hata humu jf kuna story za watu ukizisoma ni script tosha. Nadhani shida ipo kwenye taasisi yenyewe ya filamu(bongomovie) hawajui wanafanya nn. Kuna story za watu humu ukisoma unaweza tengeneza series nzuri tuu shida sisi wengine sio wasanii, mfano kuna dada alikuwaga anajiita Lara1, hadithi zake zingeweza kuwa kaseries flani ka madada wa mjini.

Sent using Jamii Forums mobile app
kweli kabisa mkuu.
 
ktk kila kazi inayofanyika kuna mtu analalamika na ktk kila kazi kuna mtu amefanikiwa kwahiyo kila kazi inahitaji mtu sahihi wa kuifanya.

Sent from my SM-G975F using Tapatalk
katika usahihi unahitajika pia usimamizi mzuri, nia, nidhamu na utiwaji moyo.
 
Shida ni mshiko wa kugharamia... hakuna ambaye ameshawishika kuwekeza pesa zake kwenye sekta hiyo. Hivyo movie tunazoziona nyingi ni watu waweze kuganga njaa tu basi
 
Shida ni mshiko wa kugharamia... hakuna ambaye ameshawishika kuwekeza pesa zake kwenye sekta hiyo. Hivyo movie tunazoziona nyingi ni watu waweze kuganga njaa tu basi
Kweli inabidi wadhamini wajitokeze na wawe na imani na usimamizi mzuri wa fedha zao wanazowekeza.
 
Back
Top Bottom