Filimbi za matundu 8 zimepotelea wapi?

Tulizitumia kwenye magwaride mashuleni enzi hizo!
Ilikuwa raha sana enzi hizo. Siku hizi haya mambo naona shuleni hakuna. Hata somo la muziki hakuna. Mtu anaitwa mwanamuziki hata kusoma music sheet hajui.
 
Kumbukumbu yako ni sahihi kabisa. Bati za betri za National!
Yah nlitumia sana

Nlipokuwa nasoma chimala shule ya msingi mbeya nlikuwa napiga sana hiyo

Nikaenda kusoma forodhan shule ya msingi kulikuwa na bendi nlikuwa natwanga sana trumpet kwenye bendi ya shule na filimbi

Ova
 
Baada ya Bongofleva kuja wanunuzi wa zana za muziki walikosekana.
 
Ilikuwa raha sana enzi hizo. Siku hizi haya mambo naona shuleni hakuna. Hata somo la muziki hakuna. Mtu anaitwa mwanamuziki hata kusoma music sheet hajui.
Ni kweli kabisa! Haya mambo hayapo kabisa siku hizi! Mfumo wetu wa elimu kwa sasa unachangia kwa sehemu kubwa kuua vipaji na ubunifu wa watoto wetu! Kuna wakati natamani enzi zile lakini ndiyo hivyo tena!
 
Halafu mi nilikuwa fa'la sana ujue!

Eti ndo nilikuwa mkali wa kupiga filimbi, dah!!!

Sema hapo juu nimesoma kuhusu filimbi za miti... dah, hizo sikuwahi kuziona aisee!! Sasa ile hollow walikuwa wanafanya fanya vp kwa mfano kuitengeneza?!
 
Yah nlitumia sana

Nlipokuwa nasoma chimala shule ya msingi mbeya nlikuwa napiga sana hiyo

Nikaenda kusoma forodhan shule ya msingi kulikuwa na bendi nlikuwa natwanga sana trumpet kwenye bendi ya shule na filimbi

Ova
Vipi bado unapiga hizo zana mkuu au umeshazisahau?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…