Film za Kiswahili

Ipan

Member
Joined
Aug 15, 2012
Posts
8
Reaction score
1
Ninapenda sana waandishi wetu walioandika vitabu mbalimbali kama: Kufa na Kupona, Je Kisasi, Dimbwi la damu, Tutarudi na roho zetu, Salamu toka Kuzimu na kadhalika. Ninachotaka kuuliza ili munipe ushauri ni kwamba, Hadithi gani ambazo zinaweza kuigizwa na zikatengeneza movie film nzuri? Watu siku hizi hawasomi vitabu sana kama zamani, zaidi utakuta wanaangalia movie tu.....changia tafadhari.
 
Hadithi (riwaya) zote ulizoweka hapo juu zaweza kutumika kutengeza filamu. Unachohitaji ni muandishi (ama waandishi) mzuri wa muswada, yaani yule aliyeisoma na kuielewa riwaya hiyo na mwenye uwezo wa kuitafsiri katika filamu. Baadae ni upatikanaji wa muongozaji mahiri atakayeweza kupanga timu nzuri na yenye uwezo ya waigizaji mahiri.

Hata nivyo kwa mawazo yangu, sidhani kama kufanya filamu za riwaya hizi kunapaswa kufanywa kama njia ya kuwapa watu uhondo kwa kuutazama na kuusikiliza badala ya kuusoma. Kwangu mimi endapo filamu ya riwaya fulani itatengenezwa basi iwe ni kwa ajili ya kuwapa watu mhamu ya kutaka kusoma riwaya, yaani, wavitafute vitabu na kuvisoma. Iwe chachu ya kuwafanya watu watake kujisomea badala ya kurahisishia kutokusoma.

#SentiZanguHamsini
 
Filamu za kibongo jina la kiingereza....filamu wametumia lugha ya kiswahili...utamaduni mixer ya marekani na Nigeria...
 
Filamu za kibongo jina la kiingereza....filamu wametumia lugha ya kiswahili...utamaduni mixer ya marekani na Nigeria...


Tatizo la watanzania wanapenda kuiga vitu bila kufikiri. Kwa kweli hata mimi sipati picha kuweka sinema jina la kiingereza simulizi kwa kiswahili. Kwa kweli inabidi tujitahidi katika hili.:A S 39:
 
Tatizo la watanzania wanapenda kuiga vitu bila kufikiri. Kwa kweli hata mimi sipati picha kuweka sinema jina la kiingereza simulizi kwa kiswahili. Kwa kweli inabidi tujitahidi katika hili.:A S 39:

Yaani acha tu.....
 
movie za kichawi ndizo zinazochezwa fresh hapa bongo,hzo nyngne kama za action magumashi tupu kwani siyo asili ya waafrka
 
moviee za kiswahilii ni kituko tuu hasa kwa wasanii chipukizii ni kama vichekesho ambavyoi vinaleta hasiraa tuu
 
Napenda sana moviee za kinigeria zinatoa maisha ya watu wote wa chini kati na rika zote
Za tanzania wanapenda kuonyesha watu wenye hadhi ya juu na kusahau ya chini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…