ukwaju_wa_ kitambo
Senior Member
- Sep 15, 2024
- 150
- 173
FINA MANGO NDANI YA POWER BREAK FAST CLOUDS FM.
Fina Mango Mtangazaji wa Redio aliye Jipatia umaarufu mkubwa katika utangazaji kwa kupitia Kipindi cha Power Breakfast cha Clouds Fm..
Enzi hizo akiwa na watangazaji wezake Gerald Hando na Paul ..
Yeye ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto watano(5) kwa upande wa mama yake, Fortunata M.Mango na watoto saba(7) kwa upande wa Marehemu baba yake,,Joseph Mango.Anaye dada mmoja na kaka watatu(3) wa kuzaliwa tumbo moja na dada mmoja na kaka mmoja wa kambo.
Alianza pilikapilika za masuala ya elimu mkoani Arusha katika shule ya Mtakatifu Constantine(St.Constantine) na baadaye kujiunga na shule ya sekondari Jitegemee jijini Dar-es-salaam kwa ajili ya masomo ya O-Level.Kisha akajiunga na shule ya Shaaban Robert ya jijini Dar-es-salaam kwa masomo ya A-Level na kuhitimu mwaka 1999.
Baada ya hapo akajiunga na Clouds FM ingawa kimasomo hakuishia hapo kwani baadaye alijiunga na FTC(Financial Training Centre) ambapo amesomea masuala ya biashara.Bado ana mpango wa kuendelea zaidi kimasomo.
Alikuwa ni Brand Manager wa kipindi cha Power Breakfast ambacho alikuwa anakiendesha kwa kushirikiana na Masoud Kipanya (KP).Kipindi kilikuwa kinarushwa kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 12 alfajiri mpaka saa 3 asubuhi.
Fina Mango pia ni mjasiriamali, yeye ndio mmiliki wa kampuni ijulikanayo kama One Plus Communication ambayo inashughulika na masuala ya Usimamizi wa Shughuli na Matukio ya Mashirika mbalimbali na Uhusiano wa Jamii (Corporate Events Management & Public Relations (PR). Ofisi za One Plus Communication zipo maeneo ya Victoria ilipo Victoria Gas Station pembezoni mwa barabara ya Ali hassan mwinyi..
.
Fina mango : Ki ukweli, the first time nimekwenda hewani haikuwa kama mtangazaji, nilikuwa kama mgeni kwenye kipindi cha M.L. Chris cha usiku – ‘Cruise to Midnight’. Lakini my first show ilikuwa on a very rainy day, nilipitiwa home, tukaja studio gorofa ya 14, Kitega Uchumi hapa, jumapili asubuhi, nikiwa napiga classics. Kipindi kilianza saa tatu asubuhi, sikumbuki for how many hours lakini nadhani kama 2 hours hivi kilikuwa. Kumbukumbu yangu ndogo yaniambia sikutetemeka wala kupanic, nakumbuka ilikuwa easy tu… the rest is history.
( katika picha )
Masoud Kipanya (wa kwanza kushoto), Fina Mango (wa pili kulia) na marehem Fredwaa wakiwa katika pozi ndani ya studio za Clouds FM.
Picha no.2
Fina Mango na Masoud Kipanya katika kitambulisho rasmi cha Power Breakfast
#funguka
Ukwaju wa kitambo
0767 542 202
Mnakumbuka Ant Virus mixtape vol..2 ya Ant virusi "Vinega" iliwataja sana ma radio presenter walio host kipindi cha Power Breakfast pale Clouds fm.
Masoud kipanya, Gerald hando na mwana dada fina mango.
Bila kusahau team xxl " b dozen & Adam mchovu.
Je? Unakumbuka nini..