Final decision

Baraka255

Member
Joined
Jun 25, 2014
Posts
73
Reaction score
14
KWA YEYOTE ATAKAE TAKA KUENDELEA NA STORY HII TAFADHALI NI TEXT HAPA 0656660223 INAITWA FINAL.DECISION NAMI NITAKUTUMIA LINK YA STORY YOTE

FILAMU YAKE ITATOKA HIVI KARIBUNI NA HII NI SEHEMU YA MWANZO.

Kanisa zima lilibaki na mshtuko waumini hawakujua nini kinaendelea kanisani hapo pindi Laurance alipo kataa kumvisha pete Norin kwa sababu ya barua aliyo ikuta ndani ya koti lake la harusi pasipo kujua ni nani aliye iweka. Msimamizi wake alijaribu kumzuia asiendelee kuisoma lakini Laurance alionyesha sura ya ukali na hasira na kuendelea kuisoma barua.

Wangu mpendwa wa nafsi;
Naomba msamaha kwa wale wote nilio wakwaza katika historia hii ya maisha yangu naomba msamaha kwa mama yangu mzazi japo umetangulia mbele ya haki miaka mingi iliyopita lakini na imani kuwa malaika wanasikia sauti yangu na jinsi nafsi yangu inavyo umia na ujumbe huu watakufikishia.

-Naomba radhi kwako mpenzi -Laurance japo -natambua kuwa -itakuwa ngumu kwako kuelewa kwa nini nimeamua kuchukua uamuzi huu mgumu. Naomba utambue tu kuwa nimeamua kufanya hivi nikiwa na akili yangu timamu na ninaamini kuwa mwisho- mwa simulizi hii sitakuwa na wewe tena maishani.

Najua jinsi gani nafsi yako inavyaumia hata mimi huku niliko moyo unaniuma na najutia sana maauzi- haya lakini naomba ukubaliane na ukweli huu na nitaomba mara baada ya kifo changu usambaze ujumbe huu kwa jamii kwa njia yoyote ile iwe magazeti, mitandao ya kijamii,blogs,website hata makala mbalimbali ili watu waweze kujifunza na kuelimika kwa kupitia mimi na wasije kuyarudia makosa kama niliyo yafanya kwenye maisha yangu.

Kipenzi rafiki yangu Regina ndiye ajuae historia yote ya maisha yangu tangu siku ya kwanza nilipowasili katika jiji hili la Dar es Salaam mpaka leo hii nikiwa nimebakiza siku moja ya kuishi juu ya uso huu wa dunia japo naye hatambui kama sitakuwa nae tena juu ya uso huu wa dunia. Na wala msiangaike kuutafuta mwili wangu baada ya kifo kwa sababu sitafia Tanzania wala nchi yoyote ya Africa.

Najua leo ni siku yako ya harusi na nilitamani kama ningeolewa na wewe kwa sababu mapenzi yetu yameanza tangu- zamani lakini nasikitika kwa kuwa malengo yote tuliyopanga tangu kipindi cha mapenzi yetu hadi uchumba wetu hakuna hata moja lililo timia.

Nakupenda sana Laurance lakini sina budi kukuacha tutaonana tena Paradiso kwenye mji wa milele mungu akipenda.Sina cha kukupatia japo nilikuahidi mengi zaidi ya niliyokupatia lakini sitaweza kufa pasipo kukuachia japo kitu cha shukrani.

Nadhani Regina atakupatia kitu kitakacho kufanya unikumbuke daima na huu ndio UAMUZI WANGU WA MWISHO.
 
Inaelekea ni stori tamu sana, hongera kwa utunzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…