Finally: Nimeanza rasmi kilimo cha miti ya mbao Iringa

Bravoooo!!!! wachache sana watakuelewa. hope tutaungana msimu ujao, pamoja na elimu itolewayo kuhusu uwekezaji wa muda mrefu watu bado wanatetemeka!! wakati mtu anaamka usingizini, atajikuta amechelewa sana. haijalishi una umri gani, time will tell.
wise
 
Mkuu umefanya vizuri mm nko katika hatua ya mwisho tutaungana mda siyo mrefu katika hiyo biashara
 
Usidanganyike. Miti ni budhaa ambayo haitakaa iishe matumizi duniani. Nampa hongera ingawa ukweli ni kuwa faida ya miti haiji baada ya muda mfupi. Badala ya kuweka fedha benki unapeleka kwenye mashamba ya miti.
 
Mungu akubariki sana Hongera sana kwa uthubutu wako huu,baadhi yetu ni waoga wa kuthubutu kufanya ,halafu ni wakwanza kulalama.
 
kilichonishangaza ni huku mufindi ndani ndani kuna hadi raia wa Kenya na Rwanda wamenunua mashamba makubwa na kupanda Miti huku watanzania tunaendelea kupiga soga kuwa hakuna ajira.
Mkuu hongera sana mimi pia nina shamba maeneo ya Itimbo ila changamoto kubwa ni moto ni majuzi tu shamba yangu imenusurika, nusura nife kwa kihoro maana miti ina miaka zaidi ya 13
 
Karibu kwenye Uwekezaji huu
 
Nimependa avatar zenu, aliyeachama kaongea kitu ambacho aliyefumba mdomo kapinga. Naungana na aliyepinga. Miti inayozuiwa ni ile ya asili, siyo ya kupanda.

Hizo avatar mwanzoni nimehisi mtu anajipinga.
 
Hongera umefanya uwekezaji mzur kikubwa zingatia tu kutunza hayo mashamba basi
 
Mkuu hongera sana mimi pia nina shamba maeneo ya Itimbo ila changamoto kubwa ni moto ni majuzi tu shamba yangu imenusurika, nusura nife kwa kihoro maana miti ina miaka zaidi ya 13
pole mkuu maana ule moto wa Itimbo niliuona na uliunguza mashamba mengi sana ....cha msingi ni kuondoa woga na kuthubutu kufanya kitu
 
Hongera broo ni kaz nzuri ..
Ningependa unipe muongozo mzima juu ya kupata shamba uko uliko ww
 
na kupau nyumba watapaua kwa mbao za zege?
 
hiyo ni biashara nzuri sana after 10 years unaweza kuvuna ukauza kila mti kwa 15,000×2250 ni zaidi ya 337,000,000 ni bonge la uwekezaji halafu watu wanalia eti serikali serikali!ebooh kufa na tufe!
Na kabla ya kuvuna anaweza akaweka mizinga ya nyuki
 
na kinachotufanya tuendelee kuwa masikini ni ubinafsi
kweli mkuu ubinafsi ni tatizo....boss wangu anamiaka 3 astaafu ila kapanda Miti zaidi ya ekari 140 ndani ya miaka 3! hapo ndo nazidi kujipa moyo na kusonga mbele.
 
Hongera mkuu hivi umeiandaa kwa ajili ya urithi wa watoto au unategemea kuvuna wewe mwenyewe huku ukiwa na kibiongo?
 
Hongera mkuu hivi umeiandaa kwa ajili ya urithi wa watoto au unategemea kuvuna wewe mwenyewe huku ukiwa na kibiongo?
itahitaji miaka 10 ifae kuvunwa. umri sio kigezo kuwa nitafaidi matunda yake coz kifo ni muda wowote bila kijali age. so long nahangaika si kwa ajili yangu tuu Bali hata wategemezi wangu wakiwemo watoto wakifaidi sio mbaya.
 
Shukran mkuu mi nshakata tamaa nna kamwembe dodo nyumbani kwangu mwaka wa Tatu huu kako palepale naona dalili ya kuja kuliwa na wajukuu
 
Shukran mkuu mi nshakata tamaa nna kamwembe dodo nyumbani kwangu mwaka wa Tatu huu kako palepale naona dalili ya kuja kuliwa na wajukuu
mkuu nazungumzia Miti ya kisasa kama pine na eucalyptus (milingoti) ambayo inatumia muda mfupi kukomaa sio ya asili...... kama milingoti ndani ya miaka 5 unaweza kuvuna mirunda au nguzo! so far unaweza kupanda Miti kwa garama ya sh 350,000 kwa ekari Baada ya miaka mitatu ukauza sh mil 1.5 kwa ekari... imagine ukiwa na ekari 20 una sh ngapi???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…