Finally, they are telling us.. !!

 
Kapinga, respect bruv, but word sh**t ain't desirable on this open forum....(unless you are in mambo ya kikubwa) you will have our browers blocked by filters at workplaces. Thanks.
 
Sasa hakuna njia ya mkato? Tulipopata Uhuru tulikuwa kwenye experiment ya kujenga Taifa, what happened? Kwanini tuliacha kulijenga Taifa na kuanza kufurahia vitu vya kuingizwa nchini? Tulikuwa na viwanda vya nguo, n.k kwanini tuliamua kuviacha na kuagiza mitumba? Tulikuwaga na SWALA sijui bado kipo au kimengia Ubia... what happened? Kwanini tuliacha kulijenga Taifa na kuanza kulitafuna halafu leo tunashangaa itatuchukua karibu nusu karne kuona matokeo ya jasho letu?
 
Wakati mwingine unaweza kuwakubali watu wenye mawazo ya 'kijinga'wanaoamini kuwa watu wanaotufukarisha watanzania ni wasomi wetu
UKISHIBA, USIMWONYESHE MUNGU TUMBO
 
Kapinga, respect bruv, but word sh**t ain't desirable on this open forum....(unless you are in mambo ya kikubwa) you will have our browers blocked by filters at workplaces. Thanks.

oops..ntakuwa nimejisahau..wer did i use the word??
 


Huyu ndiye mtaalamu mwenyewe ambaye majuzi kapewa ukuu kwa Mbwembwe na kila mara haishi matamko tata ?
 
oops..ntakuwa ntakuwa nimejisahau..wer did i use the word??

....poouwa tu, nami naona imetoweka!! no evidence or may be my browser is just playing tricks on me 🙂 ha ha
 

Good point!!
Nikisema ni ujinga kubomoa kitu unachojenga nitakuwa nimekosea?
 
Good point!!
Nikisema ni ujinga kubomoa kitu unachojenga nitakuwa nimekosea?

Nyani, tulianza vizuri kulijenga Taifa; Mwinyi akaingia akaona hakuna haja ya kulijenga Taifa, twende tuagize vitu tu yaishe.. watu wakafurahia kuwa hatimaye vitu "bwelele", tukafunga viwanda vyetu, tukabinafsisha vitu vya msingi, tukasimamisha hata JKT, na hatimaye tukabakia hatuna cha kwetu. tukaanza "kulitafuna" taifa.

Sasa tumelitafuna hadi watu washtuka; jamani mbona mnalitafuna Taifa hivyo? Kwa hiyo maneno yako hayako mbali; tulipoacha kulijenda Taifa, tulianza kulibomoa!
 
sio mawazo ya "kijinga" mimi nina hakika zaidi ya asilimia 100 ni kweli wasomi waliopewa nafasi ndio chanzo cha umaskini wa afrika hasa Tanzania.
mfano; wamezindua regulatory authority nyingi sasa hivi ,EWURA, SUMATRA n.k umewahi kujiuliza EWURA wanakata asilimia ngapi kwenye bili za wateja wa TANESCO? lengo la pesa hizo nini hasa? je EWURA inamlinda nani serikali, TANESCO au mteja(mwananchi)? nani alipaswa kubeba msalaba wa ewura, ni sahihi awe mwananchi kweli? mbona TRA hakuna makato yaliyo bayana kulipwa TRA moja kwa moja na hazina kwa upande wa pili,kama ilivyo Tanesco na ewura wanavyofanya? uko wapi mchango wa serikali kuu kwa ewura? kama bei ya umeme ni kubwa kwa mlaji wa mwisho, kwanini ewura isilipwe na serikali ama na tanesco na idara zilizo chini yake moja kwa moja? mlipaji umeme analipia ewura, biliya mwezi tanesco na service charge at the same time, nafasi ya tanesco kwa ewura mnaiona wapi? kuna kitu hapa nadhani tunajiingiza kichwa kichwa lakini wasomi wetu hamsemi na mnajidai hakuna tofauti.

service charge ya nani na kwa muda gani haya mambo ya jumla yalikwisha enzi za analog leo digital mtu hujafanyiwa service, charge inatoka wapi? hata kuandika bili ni service charge? nguzo analipia mteja gharama za kuunganishia initialy alilipa mteja wiring anafanya mteja jamani huu ni wiziiiiiii!!!! mbona benki ATM ukishatumia ndo inakatwa pesa bila kutumia inabakia ile tu ya mwisho wa mwezi hawa tanesco yao hiyo ni ipi? ewura wanahusikaje na pesa ya mtu wanayemlinda asipandishiwe bei? ni sahihi kumlipa mlinzi pesa yako ili adhibiti majambazi ambao unajua tarehe yao ya kuja kukuvamia? si ingekuwepo bodi tu ya kukutana ikiwa tanesco wanataka kuongeza bei ili ijadili kama ni sahihi ama sio sahihi? ewura kila siku wanafanya nini na bili za wateja wa tanesco ama kila siku wanatetea tanesco isitoe risiti zenye bei kubwa?

sisi ni mbumbumbu tuanze upya!!!!

naombeni mnipe makusanyo ya ewura kwa kila mwezi na tuchambua kazi zao za kila mwezi tuone uwiano wa budget na kazi zao nawahakikishi tunaibiwa tuuuuuu!!!!

nani anasema bili ya umeme tanzania ni aghali halafu anaongeza asilimia za ewura? wanatuchezea tu tunakubali tuanzie madogo haya yanayozidi bilioni 133 za EPA tuangalie 'collection sio figure'
 

Ewura wanaleta nafuu gani kwa mwananchi kama mimi na wewe kijijini ?
 
HOLD THE PRESS!!

kabla hatujaanza kutoa lawama. Naomba mnielezee kitu.

Tanzania iliaanza kusikiliza IMF na WorldBank lini? Je ni kipindi hicho hicho Mwinyi aliingia? Was it game over for Nyerere?
 
At least this guy is being honest for a change, anyway this thing is contrasting with what mkulo said couple of wks ago!! So which is which uchumi unakua au haukui???
 
At least this guy is being honest for a change, anyway this thing is contrasting with what mkulo said couple of wks ago!! So which is which uchumi unakua au haukui???

..... tumeukalia!
 
chukuwa hizo hela za EPA X 1000 wape watanzania badowatakuwa maskini. the issue here ni macroeconomic policies.. pamoja nakujenga microeconomy.

Pamoja na wizi na ufisadi wake, lakini Mkapa alijitahidi kujenga basics za macroeconomy kiasi kwamba economic indicators kama inflation na thamani ya sarafu ilikuwa stable.
Wakati anaondoka madarakani, alisisitiza kuwa kinachotakiwa kwa anayemfuatia ni kuhakikisha kuwa anaimarisha microeconomy, ili gains za macro economy zi-trickle down kwa wananchi wa kawaida.
Yaani ni kuwa alishamtafunia JK na alitakiwa kumeza tu, lakini yeye hata kumeza kumemshinda!
Inaelekea JK ni fisadi kuliko Mkapa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…