Finally, they are telling us.. !!

Mimi wote hawa nawaona kama vibudu tu. Hapa anataka kuwafanya Watanzania waone umasikini ni sehemu ya maisha yao yaani hakuta kuwa na mwanga mpaka miaka 40 ipite!!

Nakupa tano Mtanganyika nadhani umeeleza vizuri zaidi wapi CCM inakosea na ijirekebishe namna gani.
Kwa kauli ya Nduli ina maana JK ni tapeli.Alituahidi Watanzania kutuondolea umasikini katika kipindi cha miaka 5( ndo kipindi cha uongozi alichoomba).

Hii impact ya kukua kwa uchumi, kwanini inawanufaisha Wateule wa CCM,Viongozi wa serikali na wahindi wao??

Mwisho nasema CCM ni cha ambacho kinatuthibitia kwa mara ingine kuwa kimeshindwa kuwaondolea watanzania umasikini kwa kukosa Uongozi bora,Utawala bora,Usimamizi thabiti na mbinu bora za kupambana na umasikini.

80% ya watanzania wanaishi vijijini na wanategemea kilimo cha jembe la mkono. Hivi wanashindwa kuelewa kuwa ku-invest na kuweka effort kubwa kwenye sector ya kilimo pamoja na kutafuta masoko yake, kunaweza impact Watanzania wengi within 8years!! Sasa kama utawaacha hawa waendelee kulima kwa mkono unategemea lini watazalisha kwa wingi na kuboresha maisha yao.
Sasa hivi kuna njaa duniani,Tanzania tuna mabonde mazuri sana Mikoa ya Kagera,Kigoma,Rukwa,Tanga na Kigoma na baadhi ya mikoa ya kusini ambayo hayajaguswa, na tunavua za kutosha kabisa kustawisha mpunga na mahindi na ngano.Lakini tumeshindwa kutumia rasilimali hizi kutuletea neema.
CCM ni chama ambacho kimeshindwa ku-deliver kwa Watanzania, kinatafuta kila mbinu kuhalalisha kushindwa kwao.Waondoke
 
Hivi kuna matumaini gani ya kubadilisha maisha ya watu kama maafanikio ya kazi yao itakuwa ni miongo minne kuanzia sasa? Je wanaweza kufanya lolote ambalo linaweza kuwapa furaha ya matunda ya jasho lao sasa?

Hivi kujenga drainage system kwenye jiji la Dar (leo imenyesha tena mvua na mafuriko kama kawaida) hadi miaka 40 ijayo?

Hivi kuna tatizo gani la kuhakikisha kuwa kuna code za mining na mifumo ya uokoaji ya uhakika katika maeneo ya machimbo hadi miaka 40 ijayo?

Hivi aliyesema kuwa "linalowezekana leo, lisingoje kesho" alikuwa amechanganyikiwa?
 

LIFE EXPECTANCY YA MTANZANIA NI TAKRIBANI MIAKA 40 NA USHEE..KWA HIYO PROF ANA MAANA MIAKA 40 IJAYO WENGI AU WOTE WALIO HAI LEO WANAWEZA KUWA WAMEKUFA IKIWEMO YEYE...KWA HIYO HAPATAKUWA NA ATAKAYESHUHUDIA AHADI YAKE YA KUFIKIRIKA..

PLEASE GAVANA ..TUNAOMBA MIPANGO YA UCHUMI YA KUBORESHA MAISHA YA MTANZANIA KUANZIA LEO NA MIAKA IJAYO.......
 
dahh

...........anyway kama kuna mtu ana paper yake kamili aliyoi-present please atuwekee hapa tuichambue.....tujue assumptions zipi ametumia........kabla ya hizo judgements zake
 
Dola ya marekani inaporomoka siku hata siku, jee shilingi yetu ambayo imeegemezwa kwenye dola hiyo imesalimika kwenye anguko hilo la Dola?
 
nimeambiwa na gavana kupituia gazeti la last week kuwa wana njia mpya ya kupima uchumi wetu...sikuelwa au labda mimi ni mzito kuelewa.........ila kuhusu shillingi yetu sijui itakuwaje kama ipo pale pale au la........
 
Kitu muhimu zaidi ya exchange rate ni Purchasing Power Parity.

Exchange rate inaweza isituambie chochote kuhusu maendeleo ya kiuchumi,kuporomoka kwa shilingi kinadharia kunaweza kuwa na matokeo mazuri kwa exporters wanaouza nje kwa shillingi (kama tunao) kwa sababu vitu vyetu vitakuwa rahisi zaidi kununua.Vilevile Shilingi kuongezeka thamani inaweza kusababisha export kupungua kwa sababu vitu vinakuwa ghali ku export.Ndiyo maana kuna baadhi ya manufacturers wa Marekani wanafurahia dollar kushuka thamani, na importers wa ulaya wanazidisha manunuzi yao marekani, ndiyo maana China hawataki hela yao ipande thamani na wanaifanya iwe chini artificially.

Kitu cha muhimu zaidi ya short term exchange rate ni effects za long term exchange rate zinazotokea katika PPP.

Ramani hii chini inaonyesha PPP za nchi mbali mbali duniani.

http://en.wikipedia.org/wiki/Image:PPP2003-World-Borders.png
 
Shilingi imepolomoka sana kutoka USD 1163 mwanzoni mwa march na sasa inakimbilia USD 1250 kwa leo asubuhi
 
Shilingi imepolomoka sana kutoka USD 1163 mwanzoni mwa march na sasa inakimbilia USD 1250 kwa leo asubuhi

Sikubali. Tuliaambiwa na waziri wetu hazina, Mheshimiwa Mkullo "shilingi inafukuzana na dola" na gavana mpya 'Ndulu anafanya maajabu!' Mbona mbishi jamco_za?
 
Sikubali. Tuliaambiwa na waziri wetu hazina, Mheshimiwa Mkullo "shilingi inafukuzana na dola" na gavana mpya 'Ndulu anafanya maajabu!' Mbona mbishi jamco_za?

Mheshimiwa ukiwasikia wanasiasa utapumbazika sana, ni porojo tu. Wanatuzuga tu au wanawazuga wajinga. Thamani ya sarafu haimaanishi hata kidogo level ya uchumi, ukiangalia thamani ya WON ya Korea kusini kimsingi inafanana sana na thamani ya shilingi yetu lakini ukilinganisha uchumi wa Tanzania na uchumi wa Korea Kusini, ni kama utakuwa unalinganisha noti ya shilingi elfu 10 na shilingi 100. Korea wako mbali zaidi.
Siri ya kuinua uchumi wa TAnzania ipo kwenye kuimarisha uzalishaji na exports(any legal exports), hili linawezekana kabisa na limo ndani ya uwezo wetu, lakini serikali yetu haijali hilo au haifanyi kazi za maana kushughulikia hilo. Na hili unaweza kuangalia kwenye B.O.T (balance of Trade), kama kuna uwiano wa tunachopeleka nje na tunachoingiza thamani ya shilingi yetu inaweza kuwa stable au kupanda, lakini ukweli wa mambo sio huo. Hali halisi ni kuwa tunanunua kuliko tunachouza na huenda tutaendelea hivyo kwa muda mrefu kama jamaa hawataacha uzembe, ukiangalia mapato ya TRA kutokana na imports utaona ni makubwa sana, lakini waulize kuhusu exports uone kama watakujibu, watapiga blaablaa tu.
Hapa ndipo siri moja ya mismanagement ya uchumi wetu ilipo, lakini hakuna mwanasiasa atakayekubali.
 
Angalieni takwimu hizo! I guess tupo nyikani miaka arubani ya kusubiri mana kutoka mbinguni huku tukitangatanga jangwani!

 


Bongolander, niliposema Shilingi inafukuzana na dola na Ndulu kafanya maajabu nilikuwa natumia tasnifa. Yani hukuona kwamba ni kichekesho kusema Ndulu kafanya maajabu? Nilikuwa nawadhihaki wakina Mkullo!
 
Ndullu huyu huyu aliyebebwa na mafisadi wa CCM mpaka Butiama, leo anapata ubavu wa kusema "ukweli"?

Au labda tumempata Profesa wa mazingaombwe huko benki kuu? Yote yawezekana Tanzania yetu hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…