Hii imani ni kweli ipo, mimi nilisikia mwaka 2007 kutoka kwa Bosi wangu, nilienda ofisini na kumpa taarifa kuwa mke wangu amejifungu mtoto wa kike, Bosi akaniambia kuwa nitakuwa na maendeleo kwa sababu mtoto wa kike ana bahati. Sikuamini, nilijua ananitania. Sasa kwa kuwa hapa JF napo kuna watu walishasikia, labda kuna ukweli. LISEMWALO LIPO, KAMA HALIPO LAJA. Watu hawawezi kusema kitu ambacho hakipo, ndio maana hatujawahi kusikia kuwa kuna ngombe anayeruka. Lakini, kuna baadhi ya familia naona zilianza na watoto wa kike, mambo ni mabaya, nyingine zilianza wa madume, lakini mambo super. Hii ndio inasababisha nisiamini nadaharia hii.