First Class

Tobido

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2010
Posts
331
Reaction score
76
Habari Wadau.

Leo nimekuja kusisitiza jambo moja tu kwa wanachuo nalo ni kusoma kwa bidii na kuweka nia ya kupata first class coz najua ukilenga first class, upper second utaipata kwa bahati mbaya.

Ajira zimekua ngumu sana na ufaulu wako bila kujali chuo wala course ndio vitakavyokupa value na kukubeba kwenye market hivyo basi tumieni muda wenu vizuri ili msije mkajuta baadae. Ukikosa first au upper second kwa kweli unakua kwenye nafasi mbaya sana katika kupata ajira hivyo kazaneni sana wajameni. Kuna kampuni huwezi pata kazi usipokua na japo upper second. Nawaambia ili muwe na taarifa kabisa msije kuteseka baadae kutokana na kugraduate na GPA ndogo so tuliza akili soma sana na kuwa mcha MUNGU akiweka starehe, ulevi na uzinzi mbali na wewe.

Finally, niwatakieni masomo mema first year wote na wanaendelea, someni sana nasisitiza someni hata kama watu watakuona mshamba ila jua unawekeza kwa maisha yako ya baadae. Kumbuka kila mtu ametoka kwao na ukimaliza utarudi kwenu so don't let down your family.
Kwa wenzangu na mimi tuliograduate na tunatafuta kazi tueendeleeni kupambana huku tukiombeana na kutiana moyo na mwisho tutafika katika mafanikio kwa msaada wa MUNGU wetu aliejuu mbinguni.
 
Mungu aliye juu akubariki zaidi ili mdomo wako uendelee kutoa maneno yenye hekima namna hii.Naenda UDOM hakika ushauri wako nitaufanyia kazi zaidi ya unavyofikiria!
 
Mungu aliye juu akubariki zaidi ili mdomo wako uendelee kutoa maneno yenye hekima namna hii.Naenda UDOM hakika ushauri wako nitaufanyia kazi zaidi ya unavyofikiria!

Yaap kusoma ndio kila kitu just work hard na njia ya mafanikio ni nyeupe. Opportunities zinakusubiri huko mbele.
 
akhsante sana mkuu....mi namshukuru Mungu na analogia mzuri tu..mambo ya digital sijajiweka kihiiiiiiivo!
 
Mungu aliye juu akubariki zaidi ili mdomo wako uendelee kutoa maneno yenye hekima namna hii.Naenda UDOM hakika ushauri wako nitaufanyia kazi zaidi ya unavyofikiria!

Udom college gani? Ukasome sana na maneno ya Mtuflan yakae si tu kweny ubongo Bali moyoni pia
 
Fafanua mkuu misamiati yako ya TCRA cjaielewa.
siko bbm...sina mda na digital..ving'amuzi nk...mm bado analogia(old school) dona,mihogo, bada ndo msosi tofauti na kizazi cha facebook wao chocolate, chips,pizza na bagga... tungi kwa sana madem wengiiiiii nguvu hawana...ndo maana yangu
 
Teh teh nmekupata kaka. We piga shule tu hayo mengine ni kupoteza muda tu.
 
Mtuflani .... kweli umeongea!!

lakini vijana wanatakiwa kujua kuwa, kusoma sana kwa kukariri kubaya!!

soma sana,, ELEWA!

na sio soma sana,, kufaulu mitihani!

good points you have given,

mimi binafsi toka niingie chuo first year niliplan kupata upper second ki ukweli kulingana na masomo yalivyokuwa tight!!

lakini cha ajabu niliweza kuingia first class lakini kwa msuli wa ajabu na uchambuzi mkubwa sana ndugu zangu!!

someni sana,, kuna wengine hawasomi,, wanategemea lectureres! hicho kitu kipo sana huku vyuoni! nimeshuhudia binafsi!!

mwanafunzi uwezo hata wa kutoa presentation wala kuelezea kitu fulani class hana!!

lakini coursework zote kaongoza yeye, gpa kubwa anayo yeye!!

kuweni waangalifu!!
 
Last edited by a moderator:

wale ambao hawakufanikiwa kupata mkopo ama chuo hivyo kushindwa kusonga mbele na elimu ya juu UNAWASHAURI NINI mkuu!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…