First date yako ilikuwaje? Nini kilikushangaza?!

Anyway... tangazo limekaa unyama sana
Ngoja waje chap
 
LIPIA TANGAZO
 
Tuikutana kwenye basi safari ya Dar-Arusha. Mkaka mrefu mweusi halafu hb kiasi (mambo nipendayo). Mie nikisafiri sio mtu wa kuhangaika na niliyekaa nae. Nikishasalimia basi ear phone zangu natulia au nasinzia.

Kufika moshi ndio tukaanza kuzungumza baada ya kuniuliza kitu maana mie kidogo nilikuwa mwenyeji. Mwisho wa safari tukabadilishana namba za simu.

Baada ya kuwasiliana kwa miezi mitatu tukapanga kuonana kwa first date Dar hotel fulani hivi. Nilitupia nikapendeza sana. Ile kufika akawa na kazi ya kusifia tu. Tukapata chakula na vinywaji then kufika mida fulani nikamuaga, akaomba niende nae kwake tukalale. Nikamwambia asiwe na haraka maana mambo mazuri hayataki haraka. Hivyo tujipe muda zaidi wa kufahamiana.

Episode 3 ndio ilikuja kunimaliza nguvu , nilivyotoka hapo ndio ikawa nitolee. Alinitafuta sikupokea wala kujibu msg.
 
Kamdinyo unaonekana huna solo, na huna mvuto na uko desperate kuolewa kwa Mujibu wa hadithi yako.

Kosa kubwa linaloonesha value yako ni ndogo kuliko unachojaribu kuelewa, I akuwaje Mwanamke ndio uandae date kila kitu? Ulimtongoza wewe? Mbona kama ulikuwa unajipendekeza Sana? Bills zote ulipie wewe, hadi location uchgue wewe, Ile Women experience unaipataje?

Jamaa naye ni lofa tu
 
Hivi hizo first date zinahusu sisi tuliokutana mashambani ama zinahusu nyie wa mjini pekee?

Kwa sisi tuliozaliwa zamani, first date ilihusisha ule usiku wa kwanza baada ya kufunga ndoa (nyie mnaita honey moon)

Maana haikuwa rahisi kukutana na mwanamke kabla ya kumuoa, hapo kati ni wazazi pekee watakutana pamoja na washenga kuweka mambo sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…