Sky, hii role ya first lady haikuelezwa vema katika taratibu za nchi. Ni siku za karibuni imekuwa kama sehemu ya shughuli tu
Mama Maria alikuwa na jukumu la mama wa Taifa akimsaidia mzee nyumbani, ofisini n.k.
Hakuonekana kama 'first lady' wa siku hizi kwasababu alifanya majukumu yake bila taasisi rasmi na wala hakutaka media ziwe sehemu ya majukumu yake
Baada ya Mwalimu, Mzee Mwinyi naye alifuata nyayo kwa namna fulani, wakeze wakiwa na majukumu ya nyumbani na kimataifa kimya kimya bila taasisi au media
Baada ya hapo ndipo tukaanza kuona first lady wakiwa na taasisi. Kazi zao hazikuainishwa kikatiba lakini wana majukumu 'ya kitaifa'.
Ni kama utamaduni tumeiga lakini hatujautengenezea taratibu zitakazo fit na jamii yetu.
Ndiyo maana kila mmoja anakuja na taasisi yake na akiondoka anaondoka nayo
Sasa unapouliza ajira zao, sky, ajira ni ili ikupe mkate wa siku. Labda nikuulize wewe
Sky Eclat , ikiwa unafanya kazi sasa hivi na unapewa milioni 2 kwa mwezi, halafu kukawa na majukumu mengine yanayokuhakikishia milioni 10 kwa mwezi, utaitizama ajira yako kwa masikitiko?