Fidel80
JF-Expert Member
- May 3, 2008
- 21,947
- 4,470
BAADA ya kubanwa na kisha kutimuliwa kazi, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Uganda (UPDF), Brigedia Hudson Mukasa amezirejesha fedha za mishahara ya wanajeshi ambazo zilitoweka katika mazingira ya ajabu.
Taarifa kutoka nchini humo zimeeleza mapema leo asubuhi kwamba kamanda huyo wa kikosi cha tano amerejesha sh.milioni 256 ambazo zilitolewa kwa ajili ya mishahara ya wanajeshi lakini fedha hizo hazikuwafikia walengwa.
Taarifa za kurejeshwa fedha hizo zimethibitishwa na Msemaji wa UPDF, Meja Paddy Ankunda ambaye aliliambia gazeti la Daily Monitor jana kwamba kiasi cha sh. milioni 256 zimerejeshwa katika jeshi hilo na Brigedia Mukasa na akasema kwamba wanajeshi wote walioathirika na tatizo watalipwa.
Tumefanikiwa kupata Sh. milioni 256 kutoka kwa Brigedia Mukasa na wanajeshi wote walioathirika watalipwa, Meja Ankunda alisema jana.
Meja Ankunda alisema kwamba taarifa za kurejeshwa fedha hizo amezidhibitishiwa na makanda wakuu katika jeshi hilo ambao walimueleza kwamba Brigedia Mukasa alizirejesha fedha hizo kupitia akaunti ya jeshi hilo.
Hata hivyo Meja Ankunda alisema kwamba licha ya Brigedia Mukasa kuzirejesha fedha hizo jeshi hilo litaendelea na uchunguzi dhidi yake na hatua lazima zitachukuliwa dhidi yake.
Mapema mwezi uliopita Rais Yoweri Museveni alimtimua kazi Brigedia Mukasa na maofisa wengine watano katika jeshi hilo kwa tuhuma za ufujaji wa fedha za jeshi hilo.
Maofisa wengine waliotimuliwa na Rais Museveni ni Oscar Ojoket ambaye alikuwa mkuu wa kitengo cha siasa katika divisheni hiyo, Mtunza Fedha Luteni Geoffrey Mugwire mtoa vibali vya kusafiria Maaskari, James Sunday na Luteni David Birungi ambaye alikuwa Msimamizi Mkuu Mahesabu ya kikosi hicho.
Ili kuhakikisha fedha hizo ambazo zilikuwa ni za mishahara ya kikosi maalumu katika Wilaya ya Abim ambacho Serikali ilikuwa ikikitumia kwa ajili ya kupambana na waasi wa LRA pamoja na wezi wa mifugo ili kuwasaidia UPDF zinapatikana mapema, mwezi uliopita jeshi hilo iliamua kuunda tume inayoongozwa na Brigedia James Mugira na matunda yake yameanza kuonekana.