Jamani mbona Tanzania tunawasomi wengi ...naona mijadala yote ni Chenge...kikwete...mkapa... Karamagi...accacia....
jamani... hiki ni kipindi kizuri cha kudai katiba mpya ... lazima watanzania tujuwe kucheza na nyakati....
Watanzania mkombozi wa kweli ni Katiba ya Warioba tu...wala si hiyo mikataba...mnayopigia makelele ....
Unapotatua tatizo anza kwenye chanzo ... kwanza utafanikiwa milele... katiba hii ya sasa ni chanzo cha matatizo yote...
Nakuunga mkono kwa asilimia mia.Bila katiba mbadala
juhudi zote hizi za rais Magufuli zitatoweka mbele ya macho
yetu na macho ya rais mwenyewe akiwa ameishastaafu
tusipokuwa makini.
Angalia leo anahangaika kujenga viwanda,niulize
vile vilivyojengwa na Nyerere viko wapi? Si ajabu akajenga
akija mwingine asiyeona umuhimu wake akaviuza kwa bei chee.
Ni vyema kutekeleza malengo ya kitaasisi badala
ya mtu binafsi aliyepo kwa wakati huo.
Namaanisha rais ni taasisi,tusipoipa hii taasisi
mipaka ya kikatiba,tutaishia kuona akija rais mwenye
maono nchi inastawi,akija asiyejali anavunja mema yote
ya yule aliyemtangulia anafanya vya kwake.
Ni vema katiba iboreshwe,na rais alazimike
kuifuata katiba ili kulinda maslahi
mazima ya nchi yetu