Davidmmarista
JF-Expert Member
- Apr 11, 2024
- 1,367
- 2,451
Habari wadau wa Jamiiforums,
Juzi nilipata wasaa wa kuongea kwenye simu na mshakaji wangu mmoja wa Nairobi. Dah conversation Ile ilikuwa makini sana nikasema kwanini nisiwaletee wadau hapa JF na wao wajifunze.
Conversation Yetu ilikuwa kama hivi:
Mimi: "Alaah! Kumbe bado upo Nairobi? Ama ndo ushakuwa "mkali wa kurudi kimya kimya"?"
Rashid: "Bro, Nairobi si mji wa kudharau. Unapambana au unakimbia. Si unajua tena, hela haitembei na wazembe."
Mimi: "Hapo umeongea kiume. Sasa sikia, last time ulisema unafanya biashara ya sneakers na hoodies, vipi imekuwa aje?"
Rashid: "Hehee! Bro, biashara si mchezo, lakini wajanja hawalali. Leo unaamka na mia mbili kwa mfuko, kesho unaamka na mia tatu. Ukijua hesabu, kila siku ni hatua mbele."
Mimi: "Buda, si unajua vijana wengi wanajichanganya? Wanaamka asubuhi na chai ya maziwa, jioni wanarudi na chai ya kulalamika. Oooh maisha magumu, oooh sijui nifanye nini… Wanaishia kuongea kuliko kutenda!"
Rashid: "Ndiyo shida yao! Maisha si kuomba sympathy. Unajua kuna vijana mtaani wanakesha Facebook wakiandika, life is hard, badala ya kusaka solutions. Bro, mimi nishajifunza, dunia haijali feelings zako, inajali hustle yako!"
Mimi: "Hapo sawa. Ila buda, kuwa serious kidogo, kwa mfano, mimi nikiamua kuanza biashara kesho, unanishauri vipi?"
Rashid: "Sikiliza kwa makini… Kwanza, achana na wazo la nataka mtaji mkubwa. Hakuna mtu alianza na bilioni moja. Unaanza na kile kilicho mkononi. Hata kama ni duka la peremende, anza! Unaanza na vitu vidogo, alafu polepole unapanua."
Mimi: "Buda, umeongea point. Ila kuna watu wanasema hapana, biashara si ya kila mtu, mimi siko hivyoo…"
Rashid: "Hao watu ndio wale wa bro nitumie buku, nitarudisha kesho halafu kesho wakiona simu yako wanazima data. Bro, ni hivi, ukikataa biashara basi uwe na kazi yenye mshahara wa kueleweka. Kama huna kazi, wala hustle, basi uko out of options. Kwa hiyo utalialia mpaka lini?"
Mimi: "Hahaha! Umenikumbusha jamaa mmoja alichukua pesa ya project akanunua sneakers za bei mbaya, akasema ‘swag kwanza, biashara baadaye’… Saa hizi anakula ugali na chumvi!"
Rashid: "Hahahaha! Wajinga ndio waliwao, bro. Life ya mjini si fashion show. Unakula first, unavaa baadaye. Unatengeneza pesa kwanza, then unaendesha lifestyle. Usipokaa smart, utakuwa mtu wa kupiga selfie ukiwa na njaa ya mbwa."
Mimi: "Hapo sawa. Ila buda, kuna vijana wanapenda shortcuts, wakisikia crypto wanasema hapa ndo pesa iko, wakisikia forex wanasema ndio hii sasa, halafu wiki moja baadaye wanalalamika wamechomwa."
Rashid: "Bro, hizo ni mentalities za watu wavivu. Wanaamini kuna njia ya kupiga shortcut, lakini mwisho wa siku wanajikuta wamepoteza kila kitu. Hakuna shortcut kwenye kutafuta hela. Kama ingekuwepo, basi kila mtu angekuwa tajiri!"
Mimi: "Hapo sawa. Ila kuna wale vijana wa ‘bro, link please!’"
Rashid: "Haha! Hao ndo wale watu wa kutegemea kupelekwa peponi bila kufa. Wanataka link ya pesa lakini hawataki kujifunza. Wakiona mtu anaingiza mkwanja, wanataka secret formula. Hakuna formula, bro! Ni kujifunza, kupambana na kutochoka."
Mimi: "Sasa buda, una maoni gani kwa kijana ambaye anataka kuanza kupambana lakini hajui aanzie wapi?"
Rashid: "Simple. Kwanza, aache kusingizia serikali. Pili, aache kusingizia wazazi. Tatu, aanze na kile kidogo alicho nacho. Kama ana simu, aanze biashara online. Kama ana skills, ajitangaze. Kama hana kitu kabisa, atafute njia ya kujifunza. Hakuna excuse!"
Mimi: "Buda, umeongea facts tupu. Wajanja wanapata hela, wasio na akili wanalalamika."
Rashid: "Hapo ndo maana nakuambia, FISI HAFUNGI MACHO! Ukiwa mzembe, maisha yatakugonga bila huruma."
Wadau, kuna cha kuongeza hapo au ndo imetosha?!