Fiston Mayele Atua Al Ahli Tripoli kwa Mkataba wa Miaka Miwili

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga SC, Fiston Kalala Mayele, ametambulishwa rasmi kuwa mchezaji mpya wa klabu ya Al Ahli Tripoli ya nchini Libya, akitokea Pyramids FC ya Misri.

Nyota huyo wa kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), mwenye umri wa miaka 32, amewasili klabuni hapo na kusaini mkataba wa miaka miwili. Mayele alipokelewa kwa furaha na umati mkubwa wa mashabiki wa Al Ahli Tripoli waliojitokeza kwenye viwanja vya klabu hiyo na kambini kumpa mapokezi ya kishujaa.

 
Huyo angalau alikuwa mchezaji mahiri, wachezaji wengi wa kigeni wanaokuja kucheza kwenye ligi ya Tanzania ni wa kawaida sana na ndio maana wakitoka kwenda kucheza kwenye ligi bora wanachemsha haraka sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…