Fistula

Mimi k

Member
Joined
Jan 10, 2012
Posts
18
Reaction score
3
Habar jaman,

Kwa anayefaham ningependa kujua huu ugonjwa wa fistula dalili zake ni zipi na unasababishwa nini? Ningependa ni faham plz
 
Fistula ni pale sehemu mbili za mwili unapounganishwa na kamfereji kidogo. Mfano ni kama zamani ulikuwa na jipu ambalo lilikamuliwa na kupona. Sasa ile sehemu ya ndani ya jipu bado inaunganika na nje kwa mfereji mwembamba ambao unaitwa Fistula.

Ama mwanamke akiwa amepata uchungu muda mrefu bila ya kujifunguwa inasababisha ile ngozi nyembamba inayo tenganisha njia ya haja kubwa na vaginal canal kukosa damu na kuharubika. Au pia hiyo pressure ya mtoto kwenye kibofu cha mkojo na kufanya hiyo ngozi nyembamba kuoza. Vyote hivi vinasababisha kuunganika kwa kibifu cha mkojo au njia ya haja kubwa kuunganika na kusababisha fistula.

VVF- Vesicle Vaginal Fistula ni kuunganika vaginal canal na kibofu. Kwa hiyo atavuja mkojo kutoka vaginal canal bila ya stop. Very ambarasing to a woman.
RVF - Recto Vaginal Fistula. Mwanamke atakuwa anapitisha kinyesi toka vaginal canal. Mbaya sana.

Tiba ni kufanyiwa repair. Sio operation kubwa sana na inarudisha hadhi na confidance ya mwanamke.

Kinga ni kuzuia prolonged labours kwa induction. Kama pelvice hai acomodate basi C/S haraka iwezekanvyo kwa kuplan kabla.
 

Mkuu umenena vyema, Fistula ni mawasiliano kati ya sehemu mbili za mwili ambazo hazitakiwi kuwasiliana, mfano njia ya uke na haja kubwa, njia ya mkojo na uke, utumbo na nje kwenye ngozi.

fistula mara nyingi na za njia ya uke na mkojo, ama njia ya uke na njia ya haja kubwa, hizi mara nyingi ni kwa wanawake wanaopata uchungu pingamizi kwa muda mrefu.

Uchungu pingamizi maana yake ni kuwa mama na uchungu wa kujifungua, kuchwa cha mtoto kunakandamiza muda mrefu bila mtoto kuzaliwa na njia huwa ni ndogo. pale kichwa cha mtoto kinapokandamiza kwa juu huwa ni kibofu cha mkojo na kwa chini kuwa ni njia ya haja kubwa, rectum. kwa kukandamiza muda mrefu ile sehemu hukosa damu na tissue yake hufa na kutoboka na kuweka mawasiliano kati ya njia ya haja kubwa na uke ama kibofu cha mkojo na uke.

Hizo ndizo huitwa fistula, meaning a comminication between two epithelia surfaces.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…