Five killed in suspected Al Shabaab attack in Garissa

Five killed in suspected Al Shabaab attack in Garissa

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Watu hao wameuawa leo Machi 15, 2020 na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mashambulio mawili yaliyohusisha mabomu, yanayodhaniwa kufanywa na Wanamgambo wa Al Shabaab katika Kaunti ya Garissa

Watu watatu waliuawa katika shambulio la kwanza ambapo gari la kubeba Wagonjwa lililokuwa likitoka Sangailu kwenda katika hospitali ya Kaunti ndogo ya Holugho lilikanyaga bomu la kutegwa ardhini

Dereva wa gari hilo na Wanawake wawili wagonjwa waliokuwemo kwenye walifariki papo hapo huku watoto wawili wa Mwanamke mmoja wakinusurika

Aidha, katika shambulio la pili, Askari Polisi wawili waliokuwa wakienda katika eneo la tukio la kwanza wamefariki dunia baada ya gari lao walilokuwa wakisafiria kukanyaga bomu lililokuwa limetegwa ardhini
***


Five people were killed on Sunday and several others injured in two attacks by improvised explosives suspected to have been planted by Al-Shabaab militants in Garissa County.

Three people were killed in the first attack in which an ambulance traveling from Sangailu to Holugho Sub-county hospital ran over the IED.

The Ambulance driver and two female patients died on the spot, while two children belonging to one of the women who was killed, survived.

In the second attack, two police officers who were were responding to the attack were killed after their landcruiser also ran over an IED.

North-Eastern Regional Commissioner Nicodemus Ndalana has urged area residents to volunteer information on suspicious individuals in their areas.
 
IMG_20200315_235216_059.jpg
IMG_20200315_235213_620.jpg
 
Hii sio habari ya kushitua wala kusisimua kwasababu Alshabaab wanastahili kifo, tatizo ni pale wanapouliwa wakenya wasio na hatia, ambao hawana uwezo wa kujitetea wala kujilinda, wanalipa kodi wakitegemea serikali yao itawalinda, lakini wanaendelea kuuliwa karibu kila siku

Sent using Jamii Forums mobile app
Ninajua kwako sio habari ya kusisimua kwa vile wewe ndiye GAIDI wa kwanza humu.
Habari zinazokusisimua ni pale magaidi wanaua watu. Una roho kama mkaa!
 
Ninajua kwako sio habari ya kusisimua kwa vile wewe ndiye GAIDI wa kwanza humu.
Habari zinazokusisimua ni pale magaidi wanaua watu. Una roho kama mkaa!
Acha ujinga wewe, hivi tunapochinja Ng'ombe sisi binadamu hiyo ni habari?, lakini je Ng'ombe akiua mtu lazima itakua ni habari ya kushitua sana. Sababu ni kwamba Ng'ombe kuchinjwa ni haki na halali, ni jambo linalokubalika.

Kwahiyo unataka kulinganisha thamani ya uhai wa Alshabaab na thamani ya uhai wa wakenya wasio na hatia?, hiyo ndio IQ ndogo mliyonayo ninyi. Unewekewa habari kuhusu wakenya waliouliwa, eti kwa ujinga wako unaweka taarifa ya Alshabaab waliouliwa ili kuonyesha kwamba mumesawazisha kwa kulipiza, stupid.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom