Flaviana Matata aupeleka mahakamani mfuko wa PSPF akiudai milioni 165

Flaviana Matata aupeleka mahakamani mfuko wa PSPF akiudai milioni 165

chinchilla coat

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2016
Posts
5,107
Reaction score
10,969
xFlaviana.jpg.pagespeed.ic.rqRoC4dH0A.jpg


Mwanamitindo wa Tanzania anayefanya kazi zake nchini Marekani, Flaviana Matata ameushitaki mfuko wa pensheni wa PSPF mahakamani akitaka alipwe shilingi milioni 165 kutokana na mfuko kwa kosa la kukiuka mkataba wao kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania.
Flaviana ambaye ni balozi wa mfuko huo wa PSPF kupitia kwa mwanasheria wake Edward Lisso wa Law Associates Advocates wameushitaki mfuko huo kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Aidha inadaiwa kuwa Mwanamitindo huyo ameiomba mahakama iuamuru mfuko huo kumlipa kiasi cha milioni 100 ikiwa ni kama fidia kutokana na kupoteza muda na fedha nyingi ikiwa ni pamoja na kukosa fursa nyingine za kibiashara na makampuni mengine wakati akifanya mawasiliano na mlalamikiwa na ugumu alioupata wakati akifuatilia suala hilo.

Mwanamitindo huyo ameongeza kuwa anakula hasara ya kiuchumi kwa vile picha zake zinaendelea kutumika kinyume na mkataba wake na mfuko huo. Shauri hilo lipo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Magreth Bankika na litatajwa Septemba 22, mwaka huu.
 
Flaviana ameamua kuwa realistic. Angetaka fidia ya 2B kama AY na FA asingezipata.
 
Waangali wasije kugeuziwa kibao wao,ikala kwao.
 
Nikiona Kesi yeyote ya fedha fedha nakumbuka hawa majaji JAJI UTAMWA NA MAJURA MAGAFU.
 
Back
Top Bottom