Floating Bridge Unguja to Pemba U/construction

Mwiba

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
7,607
Reaction score
1,750
Ingawa linatengenezwa kwa siri lakini kwa hali lilipofikia si siri tena.



 
Sikuwa na taarifa hii kabla. Shukrani mkuu mwiba kutuhabarisha. Ni kitu kizuri kwa maendeleo. Nawapa tano kwa walau kujaribu kuanza kufanya hilo. Nchi nyingi duniani wamefanya na wamefanikiwa. Mfano, daraja la treni kati ya Uholanzi na Ubelgiji, kivuko kati ya Uingereza na Ubelgiji/Uholanzi, nk. Kwanini sisi tuwe watu wa kusimulia tu badala ya kutenda! Kufaulu au kushindwa ni sehemu ya maisha, lakini kukaa tu bila kujaribu (iwapo una resources) hakuna maana.
 

Mkuu kwa resource gani ? Hiyo 3% ya Gold au Tani 60,000 kwa mwaka za karafuu
Na kwa magari mangapi ya kupita
Acheni zenu hizo hakuna ku kama hicho for the next 20 years
 
...thubutuuu,

wangejenga la Kigamboni kwanza, BTW umbali toka unguja kwenda Pemba ni maradufu ya umbali toka Unguja kwenda Bagamoyo tu hapo, ...iwe leo wajenge daraja malindi kwenda chwaka?

...Halafu hayo maji mbona tope sana, mkondo umepita nini? 😀
 
Sasa hivi kwa akili yako kutengeneza umeme na daraja ipi rahisi.Wewe kaa usubiri uone.

Maalim Mwiba, kwa mantiki ya kujiondolea adha nzito kwanza haiingii akilini kutengeneza daraja hili badala ya matatizo ya msingi.
Hilo daraja ni kwa traffic volume ipi, na ni kwa kupeleka hiyo traffic wapi.Ndio maana kabla hata ya kujenga barabara huwa kuna feasbility study za kuonyesha economic impact ya barabara hiyo.Hili daraja lako pamoja na kuwa ni a positive thing ni kama Serikali ya Tanzania kuamua kupeleka mtu mwezini!
 
Nashauri bandiko hili lifutwe, na mleta bandiko apewe onyo kwa kubandika Tangazo feki. Ukifuatilia tovuti aliyo dokoa picha hizo Mabey & Johnson hawana mradi wowote wa ujenzi wa Daraja katika Tanzania
 

Ni kweli kabisa lakini Tanzania inakuwa kwa kasi hivyo ndoto kama hizi ni bora kuzianzisha,pengie lijengwe kutokea Bagamoyo hadi Unguja na kutokea Hale hadi Pemba naona hapo mtarizika na Muungano utakuwa umenoga.
Na kwenda mwezini ni kujiandikisha tu katika NASA jamaa kibao wamejiandikisha ndio ukaona mara anakwenda daktari mara mwalimu natumai iko siku mkulima nae atabahatika.ni chance tu ukibahatika hulipi hata ndururu.
 
Hili lingekuwa daraja lenye umbali mkubwa kuliko yote duniani, kushinda hata lile linalotaka kujengwa kati ya Djibuti na Yemen ambalo litakuwa na umbali mkubwa kuliko yote.
 
Hili lingekuwa daraja lenye umbali mkubwa kuliko yote duniani, kushinda hata lile linalotaka kujengwa kati ya Djibuti na Yemen ambalo litakuwa na umbali mkubwa kuliko yote.
Hili ni ile hali ya Tit for Tat unajua kuna mfereji wa Suez pale ambapo Afrika ilitengwa kabisa na Nchi za watu majuu. Na meli ikikatisha inalipa ndio hivyo hivyo daraja litakuwa na fedha linaingiza wakati meli inakatisha hata kule Panama nao ndio wanatia feza kwa akili kama hizi.
 
Hivi kwani April fool inakuwaga 1st of february kwa baadhi ya sehemu hapa duniani?
 
Ingawa linatengenezwa kwa siri lakini kwa hali lilipofikia si siri tena.




Chaguwa wimbo Ndugu (Mwiba) na kama itakuwa umehumiwa binafsi nahisi nikuchagulie wimbo mmoja marufu uliopigwa hapahapa nyumbani TANZANIA na vijana wetu wa BENDI YA MAKASI wimbo unaitwa siku YAKUFA naimani utakusaidia kwa kipindi hichi unachokabiliana nacho pia asante kwa kutupa tarifa za maendeleo
 

hata kama halitafika Pemba wenyewe tutalipanda na kufika linapoishia na kurudi Unguja, kwikwikwikwi. Huu kama mto malagalasi vile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…