Florah Mbasha na mumewe "NGOMA NZITO"

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Imebainika kwamba waimbaji wa muziki wa Injili nchini, Flora Mbasha na mumewe, Emmanuel Mbasha hawajapatana kama ilivyodaiwa awali na taarifa zinasema kuwa mwanadada huyo ameanza maisha yake kivyake kwa kupanga nyumba nyingine mbali na mumewe.

Habari za kuaminika toka ndani ya familia ya Flora zinasema kuwa msanii huyo amekuwa na wakati mgumu wa kumsamehe mumewe kutokana na tabia zake chafu ambazo zimekuwa zikiutesa moyo wake na sasa anang'ang'ania kumchukua mwanaye.

"Hivi karibuni iliripotiwa kuwa wanandoa hao wamepatana lakini ukweli ni kwamba hakuna kitu kama hicho,mwanamke amepanga chumba chake hapa Dar es Salaam na kumwachia kila kitu mumewe ambaye sasa ana haha kumchukua mwanaye ili aishi naye," kilisema chanzo cha habari.

Lakini upande wa pili, mume wa msanii huyo hivi karibuni alieleza kuwa ugomvi baina yao ulianza kutokana na kuchepuka kwa mkewe, huku akipeleka shutuma kwa mchungaji wa kanisa la ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ambaye ni maarufu kwa vitu ambavyo ni tofauti na huduma zake.

Emmanuel Mbasha tayari alishatoa waraka wa wazi kwenda kwa mchungaji huyo, akimtaka kukaa mbali na ndoa yake jambo ambalo bado halina mrejesho chanya kwani wawili hao Flora na Gwajima wameendelea kufanya kazi pamoja kitu kinachopelekea Emmanuel kuona bado kuna kitu kinaendelea kati yao.

Kutokana na hali hiyo, mume wa Flora amekuwa mgumu kumtoa mtoto wake akihofia kulelewa na mtu ambaye kwake anamchukulia kama adui wa familia yake.

"Imekuwa ngumu sana kwa Emmanuel kumwachia mtoto wake katika hali hii, hata kama ni wewe unamuachiaje mtoto wako kipenzi aende kwa mwanamke ambaye ni msaliti," alisema ndugu wa karibu wa Emmanuel Mbasha
 
Ni muhimu kurudi nyuma kuangalia Msingi wa ndoa yao ....ni kweli umejengwa juu ya damu ya Yesu....au..tafakali..
 
Bongo movies zote zina part 1 & 2
 
Si nilisikia kajala anavutika kwake, si ajichukulie tu lile ---- atulie!
 
Ngoja niendelee kuangalia muvi hii..sijui itafikia season ngapi yangu macho
 
Huyu dada ana lake jambo inabidi mume wake aangalie beyond that one
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…