Kuna jamaa yangu kanichekesha sana, miezi 2 iliyopita alienda Dar es Salaam, kituo cha kwanza kwake ilikuwa kuziona hizo barabara za flyover, ili apate kusafiri kwa kupitia juu.
Sasa anadai alichokiona ni tofauti kabisa, yeye alijua zina urefu kiasi kwamba unaweza kusafiri hata kilometers 4, akawa anauliza, zile ninazozionaga kwenye tv ziko wapi?
Wakamwambia ni hizo, sa mbona nikuvuka upande mmoja kwenda mwingine tu? Akaambiwa ndivyo zilivyo, kwani nyie mikoani mnajuaje?
Akasema tunajua ni barabara ndefu unaweza kusafiri hata siku nzima, jamaa alicheka Sana. Kwa mlioko Dar, tuambieni ukweli.