neema shamuhenya
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 312
- 216
BAADA ya kukabidhiwa rasmi na serikali ndege aina ya Fokker 50, Kampuni ya Ndege nchini (ATCL) imesema itaiingiza ndege hiyo katika ratiba yake ya safari za ndani ya nchi. Miongoni mwa safari hizo za ndani ni pamoja na ya Mtwara ambayo itaanza Mei 15 mwaka huu pamoja na ya Iringa, inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa ATCL, Josephat Kagirwa, aliliambia HabariLeo jana kuwa ndege hiyo ya Fokker 50 itakuwa msaada mkubwa katika kusarisha abiria wachache wanaokia 44, hivyo kuokoa mafuta na muda kama ndege kubwa zaidi ya hiyo, ingetumika kusarisha abiria wachache. Mbali na kusari kwenda Mtwara na Iringa, ndege hiyo pia kama ilivyo kwa ndege zingine za Bombardier Dash 8 Q400 na Airbus A220-300, itakuwa ikifanya safari katika mikoa ya Kigoma, Kilimanjaro, Tabora, Mwanza, Mbeya na Zanzibar.
“Ujio wa ndege hii, utasaidia kutoa huduma katika masafa mafupi, kusarisha abiria wachache ili kuokoa mafuta tofauti kama ingetumika ndege kubwa ya abiria 70 kusarisha abiria 40,”alieleza Kagirwa. Kuhusu ndege za ATCL kuanza safari za China, India, Thailand na Afrika Kusini, alisema kuwa maandalizi ya safari hizo yamekia asilimia 75 mpaka sasa.
Alisema kwa kuwa kutoka Dar es Salaam hadi India, inachukua muda wa saa tano na kwa kuwa ndege ya Airbus 220-300 ina uwezo wa kufanya safari za masafa ya kati, zinazochukua muda kati ya saa sita hadi saa sita na nusu, hivyo inaweza kuungana na ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner kusarisha abiria kwenda India na kurudi.
Kagirwa alisema kwa safari za China na Thailand itakuwa ikienda Boeing 787- 8 Dreamliner pekee, kwa kuwa ina uwezo wa kufanya safari za masafa marefu kwa ndege hiyo ina uwezo wa kusari kwa muda wa saa 18 angani bila kutua mahali popote. Kukabidhiwa kwa ndege hiyo ya Fokker 50, inaifanya ATCL kuwa na jumla ya ndege saba ikiwemo Boeing 787-8 Dreamliner, ndege mbili za Airbus A220-300 na ndege tatu aina ya Bombardier Dash Q400.
Rais Magufuli aliwahi kusema kuwa ndege nyingine ya pili aina ya Boeing 787-8 Dreamliner, itawasili nchini mwishoni mwa mwaka huu na ndege nyingine ya nne aina ya Bombardier Dash 8 Q400, nayo itawasili mwishoni mwa mwaka huu au mwaka ujao mwanzoni.