Gily Gru
JF-Expert Member
- Jul 4, 2016
- 8,632
- 23,673
Kwenye nyumba za kupanga moja hivi kuna mpangaji mmoja huwa anachukua mda mrefu kuoga, akiingia yeye lazima achukue dakika kam arobaini. Wapangaji wenzake wanachukia Sana maana inawabidi wasubiri mda mrefu atoke na wengi huchelewa asubuhi.
Mama mwenye nyumba leo kamtolea uvivu kamwambia “wewe usiku huwa unaoga na asubuhi unaoga tena alafu usiku unalala mwenyewe”. Mama mwenye nyumba kazidi kukazia “Kuna watu hata waelimishwe vipi hawawezi elewa mpaka waingie masomo ya ziada”
Jamaa akatoka bafuni anakutana uso kwa uso na mama mwenye nyumba anamsubiri nje ya bafu. Mama mwenye nyumba akamkata jicho la hasira akabwata “Mtu mwenyewe unaogea ndoo ndogo alafu unatoka na mapovu masikioni”
Jamaa kanuna siku nzima kachukizwa na majungu ya mama mwenye nyumba eti usiku huwa unaoga na asubuhi unaoga tena alafu usiku unalala mwenyewe.