mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Kamati ya corona pamoja na majukumu mengine ilipewa kazi ya kuzifanyia utafiti chanjo za corona ili kujiridhisha kwa ubora na usalama wake kabla ya kuziruhusu kutumika kwa watanzania.
Kamati hiyo ilijitokeza mbele ya watanzania wakiwa wameficha nyuso zao kwa kisingizio cha kuvaa barakoa, na wakasema chanjo hizo ni salama! Serikali kwa kuzingatia na kuuamini utafiti wa kamati ya corona wakaamua kuanza mchakato wa kuagiza chanjo za corona.
Swali: Kwa nini sasa serikali inakwepa kukubali kuwajibika kwa athari wanazoweza kupata watakaokubali kuchanjwa kama wanaamini kuwa chanjo hizo ni salama?
Naomba kuhusiana na chanjo hizi za corona lazima serikali iseme kwa wazi moja ya mambo haya mawili:
1. Kama wanakubali kuwa chanjo hizi ni salama, basi wakubali kuwajibika kwa matokeo hasi za chanjo hizo na waathirika wawe na haki ya kuidai fidia serikali mahakamani kwa madhara yanayoweza kujitokeza ya chanjo za corona.
2. Kama hilo la kwanza hawawezi kulisema, basi serikali lazima iseme wazi kuwa hawana uhakika na usalama wa chanjo hizo na atakayeamua kuchanjwa atawajibika mwenyewe kwa kukubali kwake kuchanjwa yaani "take a jab at your own risk"!
Baada ya serikali kusema moja ya mambo hayo hapo juu, hilo jambo liandikwe juu kabisa kwenye fomu ya kuridhia chanjo, na fomu hiyo iandikwe kwa kiswahili ili kila mmoja aielewe vizuri na ibandikwe kwenye mbao za matangazo kwenye kila ofisi ya serikali kuanzia serikali za mitaa na kila kwenye zahanati, kituo cha afya na hospitali zote.
Haiwezekani serikali ikatuambia chanjo ni salama halafu ikakataa kuwajibika kwa matokeo ya chanjo
Mambo ya kukataa kuwajibika huwa ni kwa chanjo za majaribio ambazo walioridhia kujitolea kwa majaribio hayo huwa wamekubali kujitoa muhanga wenyewe kwa manufaa ya utafiti. Kama serikali inatufanyia utafiti basi iseme hivyo wazi
Lakini pia majina yote ya kamati ya corona na nafasi zao yawekwe wazi. Maana tunajua jina la mwenyekiti tu, nalo tulilijua mwishoni. Historia itakuwa na jambo na kamati hii, huwezi kujua!! Wasifichwe! Kama wamefanya kazi njema wawekwe wazi ili historia iwapongeze au iwashutumu.