Naomba kwa aliye na sample ya fomu ya kupimia afya watumishi wa mahotelini na kwenye migahawa aniwekee hapa. Ukiniwekea pdf yake nitashukuru sana. Ninafungua mgahawa, sasa kupata hizo fomu wahusika wanadengua, wanataka sh 15,000/= kwa kila fomu!! sasa kwa watumishi watano nadaiwa 75,000/=(mbali na gharama ya vipimo). Nikiipata mahali nitaenda nayo ili kupunguza gharama. Natanguliza shukrani!!